Neno la Kihindi Lenye Uwezo wa Kuharibu Simu Yako ya iPhone

Neno hilo linaweza kuzima sehemu ya meseji na programu zingine
Virusi kwenye iPhone Virusi kwenye iPhone

Kampuni ya Apple inaonekana kuanza mwaka vibaya kutokana na baadhi ya matukio ambayo yamekua yakiandama kampuni hiyo siku za karibuni. Baadhi ya matukio hayo yamepelekea kampuni hiyo kuwa kwenye presha kubwa na kushindwa kutoa majibu ya haraka kwa watumiaji wa vifaa vyake.

Lakini kama haitoshi hivi karibuni, kampuni hiyo imekubwa na tatizo lingine kubwa sana kwenye vifaa vya iOS maarufu kama iPhone. Inasemekana kumegundulika aina mpya ya virusi ambavyo vinauwezo wa kuzima sehemu ya meseji kwenye simu yako yaani iMessage pamoja na programu kama WhatsApp, Facebook Messenger, Outlook ya mfumo wa iOS, pamoja na programu ya Gmail.

Virusi hivyo ambavyo vimegunduliwa na wataalam kutoka tovuti ya mobileworld vinahusisha kutumiwa meseji yenye neno moja la kihindi na endapo alie tumiwa atafungua meseji hiyo basi programu ya meseji (iMessage) huharibika na kutoku funguka tena. Aidha programu za WhatsApp, FB Messenger, Outlook ya iOS, pamoja na programu ya Gmail nazo pia zina uwezo wa kuadhiriwa na neno hilo.

Advertisement

Tayari Apple imesha pewa taarifa kuhusu hili na tayari imetoa majibu kwa kusema inafanyia kazi toleo jipya ambalo litaweza kuondoa tatizo hili ila kwa sasa kuwa makini na simu yako.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use