Usaili wa Laini kwa Alama za Vidole

Kampuni za Simu Kuanza Usajili wa Laini kwa Kutumia Alama za Vidole

Hivi karibuni kampuni za simu za hapa Tanzania zita anza kufanya usajili mpya wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole au fingerprint.

Kwa mujibu wa Taarifa hizi ambazo tumezipata kupitia SMS kutoka kampuni mbalimbali za simu ni kuwa, sehemu hiyo itakuwa kuwa kama sehemu ya ziada ili kuongeza usalama zaidi wa mwenye laini. Yani pale mtu atakapo amua kusajili laini itambidi awe na kitambulisho na itabidi pia anaye sajili aweke alama zake za vidole kwa ajili ya usalama zaidi.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni mbalimbali za simu za hapa Tanzania usajili huo wa kutumia alama za vidole unategemewa kuanza rasmi tarehe 5 mwezi wa pili mwaka huu 2018 (5/2/2018) na utaratibu huu utakua ni utaratibu ambao utatumiwa na kampuni zote zinazo sajili laini kwa ajili ya huduma za simu za mkononi hapa Tanzania. Kupata taarifa zaidi tafadhali tembelea wakala wa huduma za wateja wa kampuni ya laini unayo tumia.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Intelligent Scan kwenye Samsung Galaxy S9
Samsung Galaxy S9 Kuja na Aina Mpya ya Ulinzi wa Intelligent Scan
Next Post
Wallpaper Halisi ya Samsung Galaxy S9 Imevuja (Download Hapa) 1

Wallpaper Halisi ya Samsung Galaxy S9 Imevuja (Download Hapa)