Labfresh

Labfresh Shati la Kisasa Lisilo Chafuka Wala Kushika Madoa

Bado teknolojia inaendelea kukua kila siku, Kudhihirisha hilo wataalamu kutoka Amsterdam, huko nchini Netherlands wamefanya ugunduzi wa shati la kwanza lenye material ya pamba ambalo halichafuki wala halishiki kabisa madoa.

Labfresh ndio jina la shati hilo ambalo limetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ambayo inasaidia shati hilo kuzuia kushika madoa, bacteria pamoja na uchafu wowote naotokana na mafuta, rangi na vitu vingine kama hivyo.

https://www.youtube.com/watch?v=5MxNbnss_s8

Shati hilo ambalo hali itaji kupigwa pasi mara kwa mara , linategemewa kutoka hivi karibuni  wakati sasa wataalamu hao wakiomba support kutoka kwa watu mbalimbali ili kukamilisha hatua za mwisho za kuanza kuuza shati hilo.

Unaweza kutoa support yako pamoja na kuangalia material yaliyotengeneza shati hilo kupitia ukurasa wa kampuni hiyo kwenye tovuti ya Kickstarter.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
simu ipi bora
Simu Ipi Kati ya Hizi ni Bora Kwako kwa Mwaka Uliopita wa 2016
Next Post
Flash drive TB 2

Kingston Yaleta Flash Drive Kubwa Kuliko Zote Ina Ukubwa wa 2TB