Zuia Bando Kuisha Unapo Angalia Video Kupitia YouTube

Kupitia njia hii utaweza kusaidia bando kudumu hata unapo angaia video YouTube
Zuia Bando Kuisha Unapo Angalia Video Kupitia YouTube Zuia Bando Kuisha Unapo Angalia Video Kupitia YouTube

Ni wazi kuwa YouTube ni mmoja ya mtandao maarufu wa kuangalia video za kuelimisha, kuburushi na kufurahisha. Lakini pia kutokana na gharama za vifurushi ni rahisi sana kuishiwa bando kwa haraka pale unapo angalia video kupItia YouTube App.

Kuliona hili leo nimekuletea njia mpya ambayo natumaini inaweza kusaidia sana kuweza kupunguza matumizi makubwa ya data hasa pale unapo angalia video za YouTube kupitia app ya YouTube kwenye simu yako. Njia hii ni bora na inaweza kufanya kazi kwenye simu zote za Android pamoja na iOS.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando YouTube App

Kwa kuanza moja kwa moja fungua app ya YouTube kisha bofya kwenye picha yako ya profile ambayo huwa upande wa kulia juu.

Advertisement

Zuia Bando Kuisha Unapo Angalia Video Kupitia YouTube

 

Baada ya kubofya hapo, moja kwa moja bofya sehemu ya Settings ambayo inapatikana chini sehemu ya pili kutoka mwisho.

Zuia Bando Kuisha Unapo Angalia Video Kupitia YouTube

Baada ya hapo, utafunguka ukurasa mwingine kisha bofya sehemu ya ‘Video Quality Preferences’ ambayo inapatikana juu, option ya tatu kutoka juu.

Zuia Bando Kuisha Unapo Angalia Video Kupitia YouTube

Baada ya kubofya sehemu hiyo utaona sehemu ya kubadilisha quality za video yaani sehemu ya WiFi na Mobile Network. Sehemu hii itakusaidia kupunguza Quality ya video pale unapo angalia kwenye simu ili isichukue bando zaidi. Sasa ili kuhakikisha app ya YouTube haichukui bando zaidi unapo tazama video chagua sehemu ya Data Saver.

Zuia Bando Kuisha Unapo Angalia Video Kupitia YouTube

Hakikisha sehemu hii ya kwanza ya Video Quality on Mobile ndio inakuwa kwenye Data Saver, Sehemu hii itasaidia kuwa wakati una angalia video data haito tumika kwa wingi kwenye simu yako na hivyo utaweza kuangalia video kwa haraka lakini haito tumia data kwa wingi.

Pia ni vyema kukumbuka kuwa sehemu hii hupunguza Quality ya video hivyo kama unahitaji kuona video ikiwa angavu sana unaweza kuzima sehemu hii na kuchagua sehemu ya Auto au Higher picture quality ambayo uchukua data zaidi.

Bila shaka hadi hapo umeweza kupunguza matumizi ya data pele unapo angalia video kupitia YouTube App, kumbuka njia hizi ni sawa kwa watumiaji wote wa Android pamoja na iOS. Kama unataka kujifunza mengi kwa vitendo unaweza kujiunga nasi kuptia channel yetu ya YouTube Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use