Hizi Hapa Aina 3 za Telegram Bots Muhimu Kuzifahamu

Fanya mambo haya ndani ya app ya Telegramu bila kutumia app yoyote
Hizi Hapa Aina 3 za Telegram Bots Muhimu Kuzifahamu Hizi Hapa Aina 3 za Telegram Bots Muhimu Kuzifahamu

Telegram ni moja kati ya app za kuchati ambazo ni tofauti sana, app hii ni tofauti kutokana na sifa zake pamoja na uwezo wake wa kufanya mambo ya zaidi kupitia telegram bot.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha aina tatu za telegram bot ambazo ni nzuri sana kufahamu na nzuri sana kufanya mambo kwa urahisi na haraka. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja tukangalie bots hizi za Telegram.

Ondoa Background Kwenye Picha

Hizi Hapa Aina 3 za Telegram Bots Muhimu Kuzifahamu

Advertisement

Kama unataka kuondoa background kwenye picha yoyote kwa urahisi unaweza kutumia Telegram bot ambayo unaweza kutuma picha kupitia bot hiyo na moja kwa moja itaweza kurudisha picha hiyo ikiwa imeondolewa background. Unachotakiwa ni kutuma picha kwenye bot hiyo tu.

Fungua Telegram Bot Hii Hapa

Tengeneza Barua Pepe ya Kutumia Kwa Muda

Hizi Hapa Aina 3 za Telegram Bots Muhimu Kuzifahamu

Kama kwa namna yoyote unahitaji barua pepe ya kutumia kwa muda mfupi unaweza kutengeneza barua pepe moja kwa moja kupitia Telegram. Barua pepe hii ni ya kutumia kwa muda kama unataka kujisajili mahali na hutaki kutoa barua pepe yako. Kizuri ni kuwa unaweza kupokea barua pepe moja kwa moja ndani ya Telegram.

Fungua Telegram Bot Hii Hapa

Badilisha (Convert) Aina ya Mafaili Kati ya Picha na Video

Hizi Hapa Aina 3 za Telegram Bots Muhimu Kuzifahamu

Kama unataka kubadilisha file kati ya picha na video basi unaweza kufanya hivyo kwa kutumia telegram. Kupitia bot hii utaweza kuconvert picha na video moja kwa moja kupitia telegram. Yaani kwa mfano unaweza kubadilisha jpg kuwa png au mp4 kuwa mp3 au file lolote ambalo unahitaji. Unachotakiwa na kutuma file kwenye bot hiyo na moja kwa moja itakurudishia file hilo likiwa kwenye format unayotaka.

Fungua Telegram Bot Hii Hapa

Na hizo ndo bots za muhimu ambazo unaweza kutumia kwenye app ya Telegram, Unaweza kujaribu bots hizi kwa kubofya link chini ya maelezo kisha bofya Start kuanza kutumia bots husika. Kumbuka bots hizi zinapatikana kwenye app zote za Telegram za mifumo yote yani Android na iOS.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use