in

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Bidhaa Instagram

Angalia haya kabla ya kununua bidhaa kwenye akaunti yoyote ya Instagram

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Bidhaa Instagram
©pcmag.com

Ni wazi kuwa biashara nyingi sasa zinapatikana mtandaoni, kutokana na ongezeko la watumiaji wa Internet pamoja na urahisi wa utumiaji wa mitandao ni wazi kuwa sasa watu wengi hukimbilia mtandaoni kununua bidhaa mbalimbali.

Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo najua itakusaidia kuweza kununua bidhaa bora kwenye mitandao hasa mtandao wa Instagram.

Najua kwa namna moja ama nyingine ulishawahi kununua au kutamani kununua bidhaa Instagram, lakini ni wazi kuwa pia kwa bahati mbaya wapo ambao wametapeliwa na watu kwa kununua au kulipia bidhaa mtandaoni bila kufanikiwa kupata bidhaa yenyewe.

Sasa kupitia makala hii nitaenda kuonyesha mambo ya muhimu ambayo unatakiwa kuangalia kabla ya kuamua kununua bidhaa ya aina yoyote kwenye mtandao wa Instagram.

Njia hizi nimezitumia mwenyewe na zimenisaidia sana na nimeona nishiriki na nyie. Basi bila kupoteza muda twende kuangalie mambo haya ya muhimu.

Angalia Bei Kama Imeandikwa Kwenye Bidhaa

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Bidhaa Instagram

Ni muhimu sana kuhakikisha bidhaa unayotaka kununua imeandikwa bei, biashara nyingi siku hizi zina wauzaji ambao sio waaminifu ambao hutaka upige simu kwanza ili uambiwe bei.

Hatua hii inaonyesha kabisa biashara hii haina uaminifu, ulishawahi kuona wapi mtu anatangaza bidhaa bila kusema jambo la muhimu ambalo ni bei. Matangazo yote ya bidhaa muhimu lazima huandika bei ili kutoa nafasi kwa mnunuaji kufanya maamuzi ya haraka.

Biashara nyingi za namna hii ni madalali na huacha kuweka bei kwa kuhofia kubadilika kwa bei kwenye page zenye kuuza bidhaa hizo halisi. Hivyo ni muhimu sana kuwa makini na hili.

Weka Password Kwenye File Bila kutumia Programu

Piga Simu Kwanza Kabla ya Kununua Bidhaa

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Bidhaa Instagram

Hakikisha kwanza kabla ya kununua bidhaa unaweza kuongea na muuzaji, usichati na muuzaji kwanza kwani wauzaji wengi ambao sio waaminifu huchagua kuchati kwanza na sio kuongea na mteja.

Kuongea na muuzaji kuna onyesha kabisa kwamba namba hiyo inamilikiwa na mtu binafsi hivyo ni muhimu kufanya hivyo kwanza. Wauzaji ambao sio waaminifu huwa na namba ya WhatsApp pekee kwani hii ina msaidia yeye kushindwa kujulikana hata baada ya kufanya utapeli.

Unapo ongea na mtu unapata uwezo wa kuripoti namba yake ya simu pale ambapo itatokea umefanya biashara na mtu ambaye sio mwaminifu.

Usilipe Kabla ya Kufikishiwa Bidhaa

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Bidhaa Instagram

Watu wengi ambao wametapeliwa kwenye mtandao wa Instagram wengi wamelipa kabla ya kupokea bidhaa. Naelewa umuhimu wa kulipa kabla ya kupokea bidhaa kwa mfanya biashara lakini usikubali kufanya hivi kama biashara hiyo huijui na hujawai kufanya nayo biashara.

Ni vyema muuzaji alete bidhaa ndipo uweze kumlipa, hii inatengeneza uaminifu na hivyo kusaidia wakati mwingine kuweza kufanya biashara kwa urahisi.

Kama kuna umuhimu wa kulipa kabla ya kupokea bidhaa, hakikisha haulipi kiwango unacho takiwa kulipa na muuzaji, bali mwambie kuwa utalipia robo au nusu ya kiwango anacho taka ulipe. Mfanya biashara yoyote mwaminifu atakubali na kuleta bidhaa ndipo umalizie malipo.

Angalia Watu Unao Wafahamu Walio Fuata Page Husika

Kama kwa namna yoyote unataka kuhakikisha kuwa una nunua bidhaa halisi kwenye ukurasa ambao huja uamini kwa asilimia 100, kitu cha muhimu ni kuangalia baadhi ya watu wanao fuata kurasa hiyo.

Tofauti ya Battery za Simu Zenye Teknolojia ya Li-ion na Li-Po

Unaweza kuangalia sehemu hiyo kwa kubofya sehemu ya followed by, sehemu hii huonyesha watu wote ambao una wafahamu ambao wamefuata page husika.

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Bidhaa Instagram

Ukiona mtu yoyote unaye mfahamu unaweza kumuuliza kuhusu muuzaji huyo au ukurasa huo na kupata mawazo yake yeye anaonaje kurasa hiyo, au kama ameshawahi kununua bidhaa kupitia ukurasa husika.

Kwa kuongeza zaidi unaweza kuangalia sehemu ya Followers kuangalia kama page hiyo imefuatwa na mtu yoyote ambae akaunti yake imekuwa verfied.

Angalia Idadi ya Followers (Japo Hii Sio Muhimu Sana)

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Bidhaa Instagram

Followers sio jambo la muhimu sana bali kuna wakati inakubidi kuangalia followers unapotaka kununua bidhaa. Hii ni kwa sababu matapeli wengi huwa na akaunti zenye follower wachache sana.

Japo kuwa mtu unaweza kufanya promotion kupata followers wengi, lakini ni wazi kuwa hakuna mtu ambaye atakubali kupoteza followers wengi kwa ajili ya mtu mmoja.

Point hii siwezi kuongelea sana kwani inawezakana kabisa mtu kununua followers na kupata followers wengi kwa ajili ya kufanya utapeli, hivyo ni muhimu sana kuwa makini na hili.

Hitimisho

Kwa kuhitimisha ni vyema ufahamu kuwa njia hizi pekee haziwezi kukusaidia kujua akaunti ambayo inamilikiwa na tapeli, ni vizuri kuchukua hatua zaidi za kuchunguza akaunti kabla ya kuamua kununua bidhaa kwenye akaunti hiyo.

Hatua hizi zina weza kuwa hatua za kwanza za kujiweka salama na kujilinda dhidi ya matapeli hasa kwenye akaunti za mitandao ya kijamii zaidi ikiwa Instagram.

Kwa makala zaidi kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech, pia hakikisha unajisali kupitia kwenye channel yetu ya YouTube ili kupata mafunzo haya kwa vitendo.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.