in

Jinsi ya Kufanya Matangazo (Sponsored) Instagram (2022)

Jifunze hapa hatua kwa hatua jinsi ya kuweka tangazo instagram kwa kutumia simu

Jinsi ya Kufanya Matangazo (Sponsored) Instagram (2022)10:17

Utakubaliana na mimi kuwa instagram imekuwa ni sehemu kubwa sana ya kutafuta masoko, hii inatokana na kuwa Instagram ndio mtandao wa kijamii wenye watumiaji wengi zaidi hasa hapa Tanzania.

Kuliona hili leo nimekuletea maujanja ambayo unaweza kutumia kuweza kuonyesha matangazo au Sponsored Ad kwa kutumia akaunti yako ya M-Pesa. Njia hii ni rahisi sana na unaweza kufanya hata kwa kutumia simu yako ya mkononi, basi bila kupoteza muda zaidi twende tukangalie njia hizi.

Badilisha Akaunti Yako ya Instagram Kuwa ya Kibiashara

Hatua ya kwanza ni ya muhimu sana kwani bila hatua hii itakuwa ni ngumu sana kwa wewe kufanya matangazo kupitia Instagram. Hivyo basi hakikisha unabadilisha akaunti yako kuwa ya kibiashara kama bado hujafanya hivyo. Unaweza kufuata hatua hizi ili kuweza kubadilisha akaunti yako ya Instagram kuwa ya kibiashara.

  1. Kwenye akaunti yako ya Instagram bofya mishale mitatu iliyopo juu upande wa kulia, kisha bofya sehemu ya Settings.
  2. Baada ya hapo bofya sehemu iliyo andikwa Account.
  3. Baada ya hapo angalia mwisho kabisa ya ukurasa huo utaona sehemu iliyo andikwa Switch to Business Account.
  4. Fuata hatua zote kama inavyotakiwa hakikisha unayo akaunti ya Facebook kama huna akaunti ya Facebook kwenye hatua hizo utapewa nafasi ya kutengeneza ukurasa wa Facebook wenye jina linalo fanana na akaunti yako ya Instagram.
Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Jinsi ya Kufanya Matangazo Instagram kwa M-Pesa

Sasa baada ya kufuata hatua zote hizo utakuwa uko karibu kuanza kufanya matangazo instagram kwa kutumia akaunti yako ya M-Pesa. Hakikisha unafuata hatua hizi moja baada ya nyingine ili kuweza kufanya matangazo kwa haraka na kwa urahisi, kitu cha msingi hakikisha unapost Tangazo unalotaka kulitangaza kisha ndipo endelea kwenye hatua hizi.

Kama utakuwa umefuata hatua zote hizi basi na uhakika utakuwa umewza kufanya matangazo kupitia akaunti yako ya Instagram kwa kutumia M-Pesa. Kama kuna mahali umekwama unaweza kuuliza kupitia kwenye maoni hapo chini, kwa maujanja zaidi hakikisha una Subscribe kwenye channel yetu hapa.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

9 Comments

  1. Asante sana umenisaidia ila naomba kujua nikitaka nisitangaze facebook nitangaze instagram tu nafanyaje? Maana nalipia naona wanakata hela ya facebook na instagram ila mimi nataka kutangaza insta tu nizaidie nifanyeje