in

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 8

Spark 8 inakuja na muonekano wa tofauti kwa nyuma, tofauti na matoleo mengine

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 8

Kampuni ya Tecno hivi leo imezindua simu mpya ya Tecno Spark 8, simu hii mpya ya Spark 8 imeingia sokoni huo nchini Nigeria bila kufanyiwa matangazo au uzinduzi wa aina yoyote.

Hivi karibuni kampuni ya TECNO na Infinix zimekuwa na mtindo wa kuzindua simu nyingi za daraja la mwisho bila kuwa na matangazo wala uzinduzi wa aina yoyote.

Hivyo basi pengine tegemea kuona simu hii mpya ya TECNO Spark 8 kwenye maduka hapa Tanzania bila kuwepo kwa matangazo mengi ya simu hiyo kama inavyokuwa kwenye matoleo mengine ya Camon na Phantom.

Sifa za TECNO Spark 8

Kwa kusema hayo moja kwa moja twende tukangalie sifa za simu hii mpya, kwa kuanza na muonekano kampuni ya Tecno imekuja na msemo mpya wa “Stop at Nothing”. Msemo ambao sasa tegemea kuona kwenye simu zake nyingi.

Kwa nyuma simu hii inakuja na logo yenye maneno hayo ya “Stop at Nothing”, huku neno Spark 8 ilikiwa kwa pembeni. Pia sehemu ya kamera imakuwa pana zaidi huku ikiwa imebeba kamera mbili za Megapixel 16 na QVGA.

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 8

Sehemu hiyo pia imebeba sehemu ya fingerprint, pamoja na sehemu ya Flash ya Quad LED.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Kwa mbele TECNO Spark 8 inakuja na muundo ambao umezoeleka kwenye simu nyingi za TECNO, muundo wa kioo chenye Tear Drop notch ambayo imebeba kamera ya mbele yenye Megapixel 8. Kamera hii pia inakuja na Flash mbili moja upande wa kushoto na nyingine kulia.

Kampuni ya TECNO Yazindua Simu Mpya ya Spark 8

Kwa upande wa kioo, Spark 8 inakuja na kioo cha inch 6.5 na kioo hichi kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD.

Kwa ujumla kioo kizima kinaweza kuonyesha resolution ya hadi 720 kwa 1600 pixel. Mbali na hayo kioo hicho kinakuja na Nits ya hadi 480 ambayo hii ni kawaida ukizingatia kuwa simu hii ni simu ya bei rahisi.

Kwa upande wa sifa za ndani, TECNO Spark 8 inakuja na CPU ya Octa Core yenye speed ya hadi 2.0 GHZ, huku ikiwa inaendeshwa na Chipset ya MediaTek Helio P22 (12 nm).

Kwa upande wa RAM, Spark 8 inakuja na uwezo wa RAM hadi GB 2, huku ikiwa inasaidiwa na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 64. Hadi sasa bado hakuna taarifa za TECNO kuzindua Spark 8 yenye uhifadhi wa ndani au ROM tofauti na GB 64, ila ni wazi kuwa hilo linawezekana.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji, simu hii inatumia Android 11 Go edition, huku ukiwa na uwezo wa kupakua app zote za Google ambazo ni Go Edition.

Mbali na hayo, Simu hii mpya inaendeshwa na Battery kubwa ya 5000 mAh, ambayo ina uwezo wa kukupa hadi siku mbili za chaji bila wasiwasi kulingana na matumizi yako.

Hitimisho

Kifupi ni kuwa Spark 8 ni simu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya watumiaji wanao fanya mambo ya kawaida kwenye simu, ikiwa pamoja na kupiga simu kutembelea mitandao ya kijamii na mambo mengine.

Usitegemee kutumia TECNO Spark 8 kucheza game zenye uwezo mkubwa, kwani GPU ya PowerVR GE8320 haija tengenezwa rasmi kwa ajili ya Games nzito zenye kuhitaji kiasi kikubwa cha RAM na GPU.

Kuhusu bei unaweza kutembelea tovuti dada ya Tanzania Tech hapa kuweza kujua bei ya simu hii pamoja na simu nyingine nyingi. Kwa sasa simu hii bado haijafika hapa Tanzania hivyo pengine siku za karibuni. Tutakupa taarifa zaidi pale simu hii itakapofika hapa Tanzania.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.