Popular Now
Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026 1

Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra 2

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini 3

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini

Fahamu Sifa na Bei ya Simu Mpya ya Infinix Hot 10i 4

Fahamu Sifa na Bei ya Simu Mpya ya Infinix Hot 10i

Infinix HOT 10i ni simu iliyo zinduliwa kwa ushirikiano wa Kampuni ya simu za mkononi Infinix na Kampuni ya mawasiliano Tigo. Simu hii ya Infinix HOT 10i ina battery la ujazo wa mAh 6000 lenye kuifanya simu yako iweze kudumu na chaji zaidi ya masaa 48 lakini vile vile simu hii inapatikana kwa bei isiyozidi Tsh 320,000 ikiwa na ofa ya GB 78 za internet.

Fahamu Sifa na Bei ya Simu Mpya ya Infinix Hot 10i 5
Infinix HOT 10i inatumia Android 11 ambayo ni Android yenye kutumika kwenye matoleo mengi ya simu kwa sasa na faida yake kubwa ni namna ambavyo inaifanya simu iwe rafiki wakati wa utumiaji na hii inapelekea Infinix HOT 10i kuwa simu sahihi kwa wenye lengo la kuhamia kwenye ulimwengu wa kidijitali.

Infinix HOT 10i ni simu yenye uhakika wa picha nzuri wakati wote hata kwenye kiza kinene simu hii bado itakupa picha ang’avu Hot 10i inalifanya swala la picha kuwa rahisi kupitia Kamera 2 za nyuma zenye flash 4 huku kamera kuu ikiwa ni MP13 na kamera ya mbele MP8.

Fahamu Sifa na Bei ya Simu Mpya ya Infinix Hot 10i 6
Infinix HOT 10i imezingatia umuhimu wa kuangalia matukio mbalimbali kupitia simu endapo upo ambali na nyumbani basi kupitia wigo mpana wa kioo cha inch 6.52 unaweza kuangaza yote pasipo kupitwa na chochote.

Infinix HOT 10i ina nafasi ya kutosha ya utunzaji kumbukumbu kwa matumizi mbalimbali kama vile vitabu kwajili ya kujisomea, video za filamu, picha za safarini na mengine mengi utayafurahia kupitia memory ya GB 2 RAM, 32 ROM / 2 RAM, 64 ROM ya Infinix HOT 10i.

Fahamu Sifa na Bei ya Simu Mpya ya Infinix Hot 10i 7

Infinix HOT 10i ilizinduliwa rasmi tarehe 6/7/2021 na sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania kwa huduma ya haraka tafadhali piga 0744606222.

Previous Post
Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10 8

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti kama Twitter Ndani ya DK 10

Next Post
Kompyuta kuwa Slow

Mambo Yanayo Sababisha Kompyuta Kuwa (Slow)