Ongeza Ulinzi Kwenye Simu ya Android kwa Njia Hizi

Jaribu app hizi nzuri za kuongeza ulinzi kwenye simu ya Android
Ongeza Ulinzi Kwenye Simu ya Android kwa Njia Hizi Ongeza Ulinzi Kwenye Simu ya Android kwa Njia Hizi

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android na kwa namna moja ama nyingine ungependa kuimarisha ulinzi wa simu yako basi unasoma makala sahihi. Kupitia kwenye makala hii na kuhakikishia utaweza kufurahia app hizi kwa asilimia 100.

Kumbuka apps hizi zote ni nzuri kwa ulinzi wa simu yako na unaweza kulinda simu yako kwa namna ya tofauti na ambavyo imezoeleka kwa watu wengi. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Kuficha Picha na Video

App ya kwanza kwenye list hii ni app ambayo inakusaidia kuficha picha mbalimbali kwenye Gallery ya simu yako. App hii inaonekana kama caliculator na inafanya hesabu lakini pia inatumika kuficha picha na video kwenye simu yako. Unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutumia app hii.

Advertisement

Download App Hapa

Kujua Anaeshika Simu Yako

Kama kwa namna yoyote ukiacha simu yako mahali kuna mtu anaishika alafu ukiuliza anakataa basi app hii itakusaidia sana kuweza kujua anaeshika simu yako. App hii inauwezo wa kutuma picha ya mtu anaeshika simu yako mara kwa mara hata yule aliyeshika kwa mara moja tu akitaka kufungua simu yako. Unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutumia app hii.

Download App Hapa

Ficha SMS na Call Log

Kama kwa namna yoyote ungependa kuficha SMS pamoja na historia ya kupiga au kupigiwa simu basi app ya Private SMS and Call ni App nzuri kwako. App hii itakusaidia kuficha kabisa meseji ambazo hupendi zionekane pia itakusaidia kuweza kuficha Call Logs zako. Unaweza kujifunza jinsi ya kutumia App hii hapa.

Download App Hapa

Rudisha Vitu Ulivyofuta

Kama unajua simu yako ina mtindo wa kushikwa na mtu zaidi ya mmoja na mtu huyo anaweza kufuta kitu kwenye simu yako kwa bahati mbaya basi unahitaji app hii ya Recycle Master. App hii itakusaidia pale unapofuta kitu kisipotehe moja kwa moja kwani sasa kila kitu utakachokuwa unafuta kitahifadhi kwenye app hii kabla ya kufutwa kabisa kutoka kwenye simu yako.

Download App Hapa

Soma Meseji Bila Mtu Kujua

Kama unataka kusoma meseji za mitandao kama Facebook Messenger, WhatsApp, Instagram, Viber, Telegram, KakaoTalk, Line, Imo na VK bila mtu kujua kama uko hewani na bila mtu kujua kama umesoma meseji hiyo. App hii inauwezo mzuri sana wa kuficha Last Seen na pia una uwezo wa kusoma meseji za mitandao hiyo bila mtu kuona kama umesoma meseji hiyo.

Download App Hapa

Soma Meseji za WhatsApp Zilizofutwa

App inafuatia ni app nzuri sana ambayo inaweza kukusaidia kusoma meseji mbalimbali za WhatsApp ambazo mtu alikutumia alafu akafuta ili usiweze kusoma. App hii inauwezo wa kufanya kazi kwenye app zote za WhatsApp kwa pamoja yani WhatsApp Business pamoja na WhatsApp ya kawaida.

Download App Hapa

Na hizo ndio app nzuri nilizo kuandalia kwa simu ya leo, kama una taka kujua apps nyingine nzuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android unaweza kusoma makala yetu uliyopita kupitia hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use