in

Angalia Uzinduzi wa Samsung Galaxy S21 Ndani ya DK 12

Angalia hapa uzinduzi wa simu mpya za Samsung Galaxy S21 ndani ya muda mfupi

Angalia Uzinduzi wa Samsung Galaxy S21 Ndani ya DK 12

Kampuni ya Samsung hivi leo inazindua simu mpya za Samsung Galaxy S21 simu ambazo ni toleo jipya la simu za Samsung Galaxy S.

Kwa mwaka huu, tayari tunafahamu mengi kuhusu simu mpya za Galaxy S21, Galaxy S21 Plus na Galaxy S21 Ultra. Kama bado hujui sifa za simu hizi unaweza kusoma sifa za simu hizo kwa kubofya link hapo juu.

Lakini mbali ya hayo yapo mengi ambayo hatuyajui kama vile simu hizi mpya zinakuja bila chaja kwenye box, pamoja na mambo mengine kama vile simu ya Galaxy S21 Ultra kuja na kalamu maalum. Hayo na mengine mengi unaweza kujiunga mubashara kuangalia uzinduzi huu moja kwa moja.

Kwa habari zaidi kuhusu simu hizi mpya na nyingine nyingi zinazendelea kuzindualiwa kupitia CES 2021 unaweza kusoma hapa kupitia tovuti yetu ya Price in Tanzania. Kwa habari zaidi endelea pia kutembelea Tanzania tech kila siku.

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.