in

Angalia Channel za DSTV Kupitia Simu Bure Bila Kifurushi

Utaweza kuangalia channel mbambali kupitia simu yako ya mkononi

kuangalia dstv kwenye simu

Kama wewe ni mpenzi wa michezo, movie, Tamthilia na makala mbalimbali basi ni wazi kuwa lazima unamiliki kisimbusi cha DSTV, kama bado huna kisimbusi hicho basi pengine njia hii inaweza kukusaidia kuangalia baadhi ya channel zilizopo kwenye Kisimbusi cha DSTV bure kabisa.

Kwa kuanza basi ni vyema kujua kuwa channel za Tanzania na Afrika kama Maisha Magic Bongo na nyingine kama hizo hutaweza kuziangalia kupitia njia hii, lakini kama wewe ni mpenzi wa michezo, filamu na mengine mengi basi utaweza kufurahia njia hii kwa asilimia 100.

Kwa kuanza ni lazima uwe unatumia simu ya Android na kama tayari unatumia simu ya Android, basi moja kwa moja anza kwa kudownload app mwisho wa ukurasa huu

Kumbuka App hii haipatikani kwenye soko la Play Store hivyo ni lazima uipakue kupitia kwenye link inayo patikana mwisho wa ukurasa huu.

Baada ya kudownload na kuinstall App hiyo, sasa ingia kwenye soko la Play Store kisha pakua App ya MX Player kisha install kwenye simu yako vizuri, unaweza kupakua app hiyo pia kupitia link chini.

Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone
MX Player
Price: Free

Download Hapa

Baada ya kupakua na kuinstall vizuri App zote mbili, fungua App ya RedBox TV kisha utaona channel nyingi tofauti ambazo unaweza kuangalia kwa kubofya nembo ya Channel unayoipenda, kumbuka channel hizi zinatumia internet kwenye simu yako hivyo ni muhimu kukumbuka kununua bando kabla ya kuanza kuangalia channel hizo.

Natumaini maujanja haya yame kusaidia, kama una swali au kuna mahali umekwama usisite kutuandikia kwenye maoni hapo chini, vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Download Hapa

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

24 Comments