in

Jinsi ya Kuangalia Channel au TV za Marekani Bure Bila Kulipia

Utaweza kuangalia ESPN, HBO, NBC, Starz, TLC, Sony na channel nyingine nyingi.

Ni wazi kuwa hapa kwetu Tanzania ili kuangalia channel za TV mbalimbali ni lazima kuwa na kisimbusi na lazima ulipie kisimbusi hicho. Lakini pamoja na hayo kupitia hapa Tanzania tech tulisha kuonyesha njia ambayo unaweza kutumia kuangalia channel za DSTV bure.

Lakini kama haitoshi leo kupitia makala hii nimekuletea njia nyingine rahisi ambayo itaweza kusaidia kuangalia TV za marekani bure kabisa bila kulipia. TV au channel hizo ni pamoja na HBO, NBC, Starz, TLC, ESPN, Sony na channel nyingine nyingi sana.

Mbali ya hayo pia kupitia njia hii utaweza kurekodi channel yoyote ili bila kuinstall programu yoyote kwenye simu yako, utaweza kupata picha ya HD hata wakati ukiwa una rekodi, basi bila kuendelea kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye njia hii.

Kwa kuanza unatakiwa kudownload app hapo chini, kisha install kwenye simu yako baada ya kuinstall endelea kwa kufuata maelezo hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app moja kwa moja utaweza kuona muonekano hapo chini.

Jinsi ya Kuficha Profile Picture Kwenye App ya Telegram

Kwa kuanza utaweza kuona muonekano huo hapo juu, bofya sehemu ya Favorites kuona channel penda, au bofya Channels kuona channel zote pia bofya settings kuona mpangilio. Ili kuangalia channel bofya jina la channel kwa kubofya play.

Baada ya hapo unaweza kubofya link moja kati ya nyingi ambazo zitakuwa zinatokea mara baada ya kubofya Play. Hakikisha unachagua link yenye views nyingi zaidi.

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona channel ikianza kuonyesha picha. Ili kuweza kurekodi video kama nilivyo kwambia hapo juu unaweza kubofya sehemu ya rekodi iliyopo chini kabisa.

Baada ya kurekodi channel unayo hitaji, ili kuweza kuona channel yenye unaweza kuangalia sehemu ya Favorites kisha bofya Recording.

Kwa kufuata hatua hizo moja kwa moja utaweza kuangalia channel au TV za marekani bure kabisa bila kulipia. Kumbuka app hii inatumia data hivyo ni muhimu kuwa na MB kabla ya kutumia app hii.

Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku, pia kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua channel nzuri za YouTube za watanzania ambazo unaweza kujifunza mambo mbalimbali.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment