Sasa Chagua Comment Gani Ionekana Juu Kupitia Instagram 1

Sasa Chagua Comment Gani Ionekana Juu Kupitia Instagram

Mtandao wa Instagram hivi karibuni umewezesha sehemu mpya ya Pin Your Favorite Comments ambayo inaruhusu watumiaji wake kuweza kuchagua ni comment gani ziweze kuonekana juu pale unapo post picha au video kupitia mtandao wa Instagram.

Sasa Chagua Comment Gani Ionekana Juu Kupitia Instagram 2

Kwa mujibu wa mtandao wa Instagram, sehemu hiyo mpya itakuruhusu kuchagua hadi comment za watu watatu ambazo unataka ziweze kuonekana chini ya picha au video yako kupitia mtandao huo.

Ili kuweza kuchagua comment unazotaka zionekane za kwanza, unaweza kushikilia kwa muda comment unayotaka na utaona sehemu ya Pin Your Favorite Comments ikitokea kwa juu, au unaweza kuslide comment hiyo kwenda kushoto na moja kwa moja unaweza kuona sehemu hiyo mpya ya pin.

Sasa Chagua Comment Gani Ionekana Juu Kupitia Instagram 3

Kama unataka kuondoa comment hiyo basi unaweza kushikilia tena comment unayotaka kuondoa na moja kwa moja utabofya sehemu ya pin na kisha chagua Unpin kuondoa comment hizo juu.

Sehemu hii kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wote wa mtandao wa Instagram, kama sehemu hii bado haipo kwenye programu yako ya Instagram basi hakikisha una update app ya Instagram kupitia soko la Play Store au App Store.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Mtandao wa Kijamii wa TikTok Kusitishwa Hong Kong 4
Mtandao wa Kijamii wa TikTok Kusitishwa Hong Kong
Next Post
Tetesi : Baadhi ya Simu za Samsung na iPhone Kuja Bila Chaja 5

Tetesi : Baadhi ya Simu za Samsung na iPhone Kuja Bila Chaja