in

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Haya hapa yote ya muhimu unayotakiwa kujua kuhusu simu mpya ya Note 10

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye hapo jana kampuni ya Samsung ilizindua rasmi simu mpya za Galaxy Note 10 pamoja na Galaxy Note 10+ simu ambazo zinakuja na maboresho zaidi ya muundo kuliko Galaxy Note 9 ya mwaka jana 2018.

Samsung Galaxy Note 10

Kwa mwaka huu Samsung imekuja na Matoleo mawili ya Galaxy Note 10, tofauti na miaka mingine ambayo tumezoea kuona toleo moja tu la Note. Galaxy Note 10 ndio toleo la kwanza la simu hii huku Note 10+ ikiwa ndio toleo la pili (kubwa) la simu hizi za Samsung. Kwa kuanza hebu tuangalie simu hii ya Galaxy Note 10.

Kioo

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Bila kupoteza muda tukianza na Galaxy Note 10, hii inakuja na kioo cha inch 6.3 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Dynamic AMOLED huku kikiwa na resolution ya hadi pixel 1080 x 2280. Mbali na hayo kioo hicho kinakuja na teknolojia za ziada kama vile HDR10+, Always on pamoja na glass ngumu ya Corning Gorilla Glass. Chini ya kioo hicho kuna Sensor ya fingerprint ambayo inakusaidia kufungua simu yako kwa kutumia alama za vidole.

Kamera ya Mbele

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Tukiwa bado upande wa mbele, kwa juu Galaxy Note 10 inakuja na kamera moja ya selfie yenye Megapixel 10, ambayo inakuja na uwezo wa kurekodi video za hadi pixels 1440p@30fps. Kamera hiyo pia inakuja ikiwa inasaidiwa na teknolojia za Dual video call pamoja na Auto-HDR.

Kamera za Nyuma

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Kwa nyuma Galaxy Note 10 inakuja na kamera tatu, huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 12 ambayo hii ni wide lens, huku nyingine mbili zikiwa zinakuja na Megapixel 12 ambayo ni telephoto lens pamoja na Megapixel 16 ambayo ni ultrawide lens. Kamera zote hizi kwa ujumla zinaweza kuchukua video za hadi 4K ambayo ni sawa na kusema simu hii inauwezo wa kuchukua video za 2160p@60fps, 1080p@240fps pamoja na 720p@960fps.

Muundo

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Kwa upande wa muundo wa Galaxy Note 10 imebadilika sana huku Samsung ikiwa imefanya mabadiliko makubwa ikiwa pamoja na kuondoa kitufe cha kuwasha na kuzima simu ambapo sasa inakubidi kuzima simu kwa kuingia kwenye sehemu ya Notification panel ndani ya simu. Upande wa kulia ambapo ndipo huwa kitufe cha kuwasha na kuzima simu sasa ni mweupe kabida na hauna kibonyezo chochote. Upande wa kushoto kuna kitufe cha kuongeza na kupunguza sauti na kitife ambao kinawasha programu ya Bixby ya Samsung.

Simu hii pia inakuja na teknolojia za kuzuia maji na vumbi IP68, huku ikiwa na uwezo wa kukaa kwenye maji ya mita 1.5 kwa muda wa dakika 30.

Kalamu ya Galaxy Note 10

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Kwa upande wa kalamu ambayo ndio inafanya simu hizi za Note kuwa Note, Samsung imefanya maboresho kadhaa ambapo sasa kalamu hii inakuja na uwezo wa kuendesha kamera bila kugusa kamera kwa kutumia kalamu hiyo. Kwa mfano pale unapo chukua kalamu hiyo na kuizungusha hewani kamera ya simu hiyo huweza kuwaka na unaweza kuchagua kamera ya mbele au ya nyuma kwa kuzungusha tena kalamu hiyo hewani.

Sifa za Galaxy Note 10

Kwa upande wa Sifa Galaxy Note 10 inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya Exynos 9825 (7 nm) – EMEA/LATAM huku matoleo ya simu hii ambayo yatapatikana kwa nchi za china na Marekani yakiwa na processor za Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) – USA/China. Processor hizi zinasaidiwa na RAM ya 8 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 256, Simu hii haina sehemu ya kuweka memory card hivyo natumaini GB 256 zinakutosha.

Mbali na hayo simu hii ni sio haba kwenye kucheza Game kwani inakuja na GPU ya Mali-G76 MP12 – EMEA/LATAM, huku matoleo ya China na marekani yakiwa yanakuja na GPU tofauti ya Adreno 640 – USA/China.

Mfumo wa Uendeshaji

Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji Galaxy Note 10 inakuja na mfumo wa Android 9 Pie, huku ikiwa na mfumo wa Samsung wa One UI ambao umeboreshwa zaidi. Vilevile Samsung inakuja na mfumo wa Samsung Dex, mfumo ambao unakuruhusu kutumia Simu hii kwenye kioo cha kompyuta kwa kuchomeka simu hiyo kwa kutumia waya maalum.

Uwezo wa Battery

Kwa upande wa battery Note 10 inakuja na battery ya Li-Ion 3500 mAh, battery ambayo inakuja na teknolojia Fast battery charging ya hadi 25W. Mbali na hayo Note 10 pia inakuja na teknolojia ya Fast Qi/PMA wireless charging ya hadi 20W huku ikiwa inatofautiana kwa baadhi ya nchi.

Viunganishi na Mengine

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Galaxy Note 10 inakuja na radio kwa simu zitakazo patikana nchin marekani na China, lakini kwa simu zitakazo patikana hapa Afrika inawezekana kabisa isiwe na Radio. Simu hii pia inakuja ikiwa haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, na sasa inakubidi kutumia headphone za Type C ambazo zinachomekwa sehemu moja na sehemu ya chaji ambayo inatumia USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10

Simu hii pia inakuja na Wifi ya Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac/ax, dual-band yenye uwezo wa Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth ya 5.0, A2DP, LE, aptX pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO. Simu hii pia inakuja na teknolojia ya NFC. Mbali na hayo Note 10 inakuja na Sensor za Fingerprint (chini ya kioo), accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer na SpO2. Galaxy Note 10 inakuja na rangi tatu za kuchagua za Aura Glow, Aura White pamoja na Aura Black

Bei ya Galaxy Note 10

Kwa mujibu wa Samsung, bei ya Galaxy Note 10 inatarajiwa kuuzwa kwa dollar za marekani $988 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 2,273,000 bila kodi kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. Kumbuka kwa Tanzania na Afrika nzima bei ya simu hii inaweza kubadilika kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Na hizo ndio sifa na bei ya Galaxy Note 10, kama unataka kujua sifa kamili za Galaxy Note 10+ basi unaweza kusoma makala inayofuatia hapa.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments