Ubunifu wa Kitanzania Teknolojia ya Kuzuia Wizi wa Magari

Inawezekana hii ndio dawa ya wizi wa magari Tanzania..?
Ubunifu wa Kitanzania Teknolojia ya Kuzuia Wizi wa Magari Ubunifu wa Kitanzania Teknolojia ya Kuzuia Wizi wa Magari

Habari siku ya leo kutoka Tanzania, Wabunifu wa teknolojia kutoka hapa nchini wamekuja na mfumo mpya ambao unaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kuzuia wizi wa magari hasa hapa nchini Tanzania.

Wakihojiwa kupitia millardayo, wabunifu hao ambao ni wakazi wa jijini Dar es salaam wamekuja na teknolojia hiyo ambayo itamuwezesha mtu kuzima na kuwasha gari lake popote pale alipo, ikiwa pamoja na kupata data za mahali gari lake lilipo kupitia GPS pamoja na mambo mengine mengi.

Mfumo huo ambao unafungwa kwenye gari, kwa sasa tayari unatumika kwenye magari zaidi ya 200 hapa nchini Tanzania huku magari hayo yote yakiwa salama kutokana na kusaidiwa na mfumo huo ulio buniwa na vijana wa kitanzania. Kujua zaidi kuhusu mfumo huo angalia video hapo chini.

Advertisement

Je nini maoni yako kuhusu ubunifu huu, unadhani unaweza kusaidia kupunguza uwizi wa magari hasa hapa kwetu Tanzania..? Tuambie kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use