Ripoti : Huawei Yauza Simu Nyingi Kuliko Kampuni ya Apple

Simu ya Huawei P20 ndio imeuza nakala nyingi kuliko Hata iPhone X
kampuni ya Huawei kampuni ya Huawei

Kampuni ya Huawei imetangazwa kuwa imeuza nakala nyingi za simu kwenye nusu ya pili ya mwaka 2018 kuliko kampuni ya Apple. Kwa mujibu wa ripoti kutoka IDC kampuni ya Huawei imeuza nakala zaidi ya milioni 54 ukilinganisha na kampuni ya Apple ambayo yenyewe imesafirisha nakala milioni 41.3 kwenye nusu ya pili ya mwaka huu 2018.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa, Kampuni ya Samsung ndio imeshika namba moja kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 71 ikifuatiwa na kampuni hiyo ya Huawei na kisha kampuni ya Apple ambayo yenyewe imeshikilia nafasi ya tatu.

Hata hivyo inasemekana kuwa Huawei imeshika nafasi hiyo baada ya kutoa simu zake za Huawei P20 na Huawei P20 Pro ambazo ndio zinasemekana kuuza nakala nyingi zaidi kutoka kampuni hiyo. Vilevile Samsung inaendelea kushilia nafasi nzuri kwa kusafirisha nakala milioni 73, lakini bado kampuni hiyo wiki hii imebainisha kuwa mauzo ya simu za Samsung Galaxy S9 hayako vizuri sana kutokana na uhitaji wa simu hizo kupungua kwa kiasi kikubwa.

Advertisement

Simu zote mbili za Huawei P20 na Samsung Galaxy S9 ni simu zenye maboresho sana kwenye upande wa kamera, huku Huawei ikija na kamera tatu kwa nyuma wakati Galaxy S9 ikija na kamera mbili zenye teknolojia mpya ya kuweza kupiga picha vizuri zaidi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use