in

Tetesi : Samsung Kuja na Simu ya Kwanza Kwaajili ya Game

Wapenzi wa Samsung sasa Jiandaeni na simu hii mpya..

Simu ya Samsung ya Game

Ulimwengu wa Game ni sekta ambayo inatengeneza pesa nyingi sana siku hizi, ndio maana sio ajabu kuona kampuni kama Samsung ikijitayarisha kuingia kwenye upande huo kwa kuja na smartphone yake ya kwanza ambayo itakuwa maalum kwa wapenzi wa game duniani.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, bado hakuna taarifa zaidi kuhusu simu hiyo ila kwa mujibu wa mvujishaji maarufu wa nchini china MMDDJ_ , simu hii inatarajiwa kuzindulia siku za karibuni na inasemekana kuja na jina la Galaxy X na inasemekana kuja na processor yenye nguvu kwaajili ya game ya Snapdragon 845 chipset.

Kampuni nyingi za simu tayari zina smartphone ambazo ni maalum kwaajili ya Game, siku za karibuni tuliona simu mpya ya Razer Phone ambayo yenyewe inakuja na laptop yake kwaajili ya kucheza game. Vilevile pia tuliona simu ya Xiaomi Black Shark ambayo pia ni simu kwaajili ya Game ambayo nayo pia inakuja na uwezo mkubwa na wakipekee. Sasa ni zamu ya Samsung ambayo nayo inatarajia kuja labda Galaxy X ambayo bila shaka itakuwa ni simu bora zaidi kwaajili ya wapenzi wa game.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.