Tetesi : Instagram Kuja na App Mpya ya Kuuza na Kununua

App hiyo mpya ya kuuza na kununua inategemewa kupewa jina la IG Shopping
Sehemu mpya ya IG Shopping Sehemu mpya ya IG Shopping

Habari za hivi karibuni kuhusu mtandao wa Instagram zinasema kuwa, Baada ya instagram kuja na IGTV sasa Instagram iko kwenye hatua za awali za kutengeneza App mpya ambayo itakuwa ni sehemu ya mtandao Instagram lakini itakuwa ni maalum kwaajili ya wafanyabiashara pamoja na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kupitia mtandao wa Instagram.

Habari kutoka kwenye mtandao wa The Verge zinasema kuwa, kupitia msemaji mmoja ambae anajua kuhusu swala hilo wamebaini kuwa, App hiyo mpya inawezekana kupewa jina la IG Shopping na itaruhusu watumiaji kuweza kununua bidhaa au kuuza moja kwa moja kupitia Instagram kwa kutumia akaunti zao hizo hizo za mtandao huo.

Kwa mujibu wa Instagram, akaunti zaidi ya milioni 25 ndani ya mtandao wa instagram zinamilikiwa na biashara mbalimbali, huku akaunti zaidi ya milioni 2 kati ya hizo zikiwa zinatumia matangazo ya kulipia ya mtandao huo kwaajili ya kufikia wateja mbalimbali. Mbali na hayo Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Facebook Sheryl Sandberg, alisema kuwa, katika kila watumiaji wanne au watano wa mtandao wa Instagram, lazima mtumiaji mmoja kati ya hao wanafuata (Follow) akaunti moja ambayo ni akaunti ya kibiashara, kutokana na hayo ni wazi mtandao huo sasa umeanza kuunganisha wafanya biashara mbalimbali duniani.

Advertisement

Kwa sasa inasemekana sehemu hiyo bado iko kwenye hatua za awali sana za matengenezo hivyo pengine itachukua muda kidogo hadi kukamilika kwa sehemu hiyo ya IG Shopping ambayo inategemewa kuwa ni maalum kwa wauzaji na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kupitia Instagram.

Nini maoni yako kuhusu sehemu hiyo mpya inayokuja hivi karibuni..?, unahisi inaweza kuwa msaada kwa wauzaji na wanunuaji wa bidhaa mbalimbali hapa Tanzania..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use