Tetesi : Hizi Hapa Picha za Simu Mpya ya Huawei Mate 20 lite

Picha za muonekano wa simu mpya ya Huawei Mate 20 Lite
Picha za Huawei Mate 20 Lite Picha za Huawei Mate 20 Lite

Kampuni ya Huawei inajianda kuja na toleo la simu yake mpya ya Huawei Mate 20, Wakati zikiwa zimebakia siku chache tayari tetesi za simu hiyo mpya zimeanza rasmi. Kupitia mitandao mbalimbali, tumefanikiwa kupata picha ambazo zinasemekana ni moja kati ya picha za toleo la simu mpya ya Huawei Mate 20 Lite ambayo inategemea kuzinduliwa kama toleo la simu ya Huawei Mate 20.

Kwa mujibu wa picha hizo, Huawei Mate 20 Lite itakuja na kamera mbili kwa nyuma ambazo zitakuwa kwa mtindo wa wima huku kwa chini yake kukiwa na sehemu ya Fingerprint. Simu hiyo pia inaonekana kuja na kioo chenye ukingo wa juu maarufu kama Top Notch.

Simu hii hiyo ya Huawei Mate 20 Lite pia inasemekana kuja na kava la Glass kwa nyuma, tofauti na simu ya Mwaka jana ya Huawei Mate 10 ambayo ilikuwa na kava la chuma. Simu hii pia inakuja na rangi mbili za Black pamoja na Gold.

Advertisement

Kwa upande mwingine bado hakuna taarifa zaidi kuhusu sifa za simu hii, ila endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi juu ya ujio wa simu hii pamoja na sifa kamili.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use