Kutana na “Razer Phone” Hii Ndio Simu Bora kwaajili ya Game

Ifahamu simu inayosemekana kuwa ni bora kwa kucheza game..
Razer Phone Razer Phone

Kuna watu wengi sana wanapenda simu (smartphone) zenye uwezo mkubwa (kuanzaia kioo mpaka sifa) sababu ya kucheza game, kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda kucheza game kwenye simu basi simu hii ni moja kati ya simu ambazo ni muhimu sana wewe kuwa nayo au kuifahamu.

Kwa wale ambao hawaijui kampuni ya Razer, hii ni kampuni maarufu sana kwa utengenezaji wa kompyuta na vifaa maalum vya game. Kampuni hii ilianzishwa na Min-Liang Tan pamoja na Robert Krakoff huko nchini Singapore lakini kwa sasa makao makuu ya kampuni hii yapo nchini marekani kwenye mji wa California.

Advertisement

Mpaka sasa kampuni hiyo imesha wahi kutoa kompyuta mbalimbali za game ambazo ni ghali sana ikiwepo pia laptop yenye vioo vitatu iliyopewa jina la Project Valerie ambayo ilitangazwa rasmi mwanzoni mwa mwaka huu kwenye mkutano wa CES wa Mwaka 2017.

Kwa upande wa simu mwaka huu ndio mara ya kwanza kabisa kwa kampuni hiyo kujikita kwenye biashara ya simu za mkononi maarufu kama Smartphone na kwa sababu kampuni hii imekua ikitoa kompyuta zenye uwezo mkubwa pamoja na muundo wa aina yake, hebu sasa tuangazie simu hii kwa undani kidogo.

  • Uwezo wa kioo – inch 5.7 huku kikiwa na teknolojia ya IGZO IPS LCD pamoja na uwezo wa kuonyesha rangi zaidi ya milioni 16.
  • Mfumo wa uendeshaji – Android 7 au Android Nougat.
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.35 GHz Kryo & 4×1.9 GHz Kryo) huku ikiwa imetengenezwa kwa Qualcomm MSM8998 Snapdragon 835
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 huku ikiwa na uwezo wa kuweka memory card mpaka ya GB 256
  • Uwezo wa RAM – GB 8
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye teknolojia ya autofocus
  • Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja inayo megapixel 12 na nyingine inayo Megapixel 13 huku ikiwa na uwezo wa (f/1.75, PDAF & f/2.6, PDAF), 2x optical zoom pamoja na flash mbili za LED (dual tone) flash.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint ambayo ipo kwa pembeni
  • Uwezo wa Bluetooth – 4.2, A2DP, LE
  • Pini ya Headphone – Haina pini ya kuchomeka headphone inatumia USB
  • Uwezo wa WiFi – 802.11 a/b/g/n/ac, dual-band, WiFi Direct, hotspot
  • Uwezo wa Battery – 4000 mAh battery hii haitoki na imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion, pia simu hii inayo teknolojia ya Fast battery charging (Quick Charge 4+).
  • Rangi – Simu hii inakuja na rangi moja nyeusi.
  • Bei – dollar za marekani $699 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,571,701.50 hii ni kwa mujibu wa viwango vya fedha vya leo kumbuka bei inaweza kuongezeka.
  • Upatikanaji – Simu hii inapatika kuanzia tarehe 17 November.

Na hiyo ndio simu mpya ya Razer Phone ambayo imetoka rasmi hapo jana, tuambie maoni yako unaonaje simu hii na je ungependa simu ambayo ni maalum kwa kucheza game..? tujulishe kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Wired

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use