Kampuni ya Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Xiaomi Mi 8

Inakuja na Kamera mbili nyuma, GPS Mbili, na Fingerprint kwenye kioo
Sifa na Bei ya Xiaomi Mi 8 Sifa na Bei ya Xiaomi Mi 8

Baada ya tetesi za muda mrefu hivi leo Kampuni ya Xiaomi ime sherekea miaka minane ya kuanzishwa kwake kwa kuzindua simu mpya ya Xiaomi Mi 8. Simu hiyo mpya inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 845, kamera mbili, GPS mbili, na pia hii ndio simu ya kwanza kutoka kampuni ya Xiaomi kuwa na ukingo wa juu maarufu kama Notch.

Simu hiyo iliyozinduliwa na CEO wa kampuni ya Xiaomi, Lei Jun, inakuja na kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na uwezo wa Megapixel 12 yenye (f/1.8, 1.4µm) na nyingine pia ikiwa na Megapixel 12 (f/2.4, 1.0 µm) lakini yenye uwezo wa telephoto lens. Vilevile kamera hizi zinakuja na teknolojia ya AI au Artificial Intelligence ambayo inauwezo wa kutambua Maonyesho (Scenes) zaidi ya 200, pia inatumia teknolojia ya 4-in-1 pixel binning ambayo inasaidia kufanya kamera za simu hiyo kuchukua picha vizuri kwenye mwanga mdogo.

Kwa upande wa kamera ya mbele, Xiaomi Mi 8 inakuja na kamera moja ya Megapixel 20 yenye f/2.0 aperture ambayo nayo pia inakuja na teknolojia ya AI kwa ajili ya kuchukua picha za portrait selfies na AI Beautify. Kwa mbele simu hiyo pia inakuja na sensor za kutambua uso ambazo zina uwezo wa kufanya mtumiaji aweze kufungua simu kwa kutumia uso.

Advertisement

Mbali na hayo Xiaomi Mi 8, pia imekuwa ndio simu ya kwanza kuwa na uwezo wa GPS mbili hii ikiwa inaipa uwezo mzuri zaidi wa kutambua kwa usahihi mahala simu hii ilipo. Mbali na hayo kitu kingine cha kujua kuhusu simu hii ni pamoja na kuwepo kwa toleo lingine la simu hii linalo itwa Explorer Edition ambalo lenyewe linakuja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint ambayo inapatikana kwa mbele juu ya kioo, huku kwa nyuma ikiwa na kava ambalo lina onyesha kwa ndani (Transparent).

Sifa nyingine za simu hii mpya ya Xiaomi Mi 8 ni kama zifuatazo.

Sifa za Xiaomi Mi 8

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.21 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2248 pixels (~402 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 385 Silver), Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu, moja itakuwa na ukubwa wa ndani wa GB 64 na nyingine GB 128 pamoja na nyingine GB 256 zote zikiwa hazina uwezo wa kuongezewa na memory card (Haina Sehemu ya Memory Card).
  • Ukubwa wa RAM – GB 6 kwa Simu zote
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 20, yenye 20 MP (f/2.0, 1.8µm), 1080p.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye uwezo wa (f/1.8, 1.4µm, 4-axis OIS, dual-pixel PDAF) na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye (f/2.4), huku zote zikiwa na uwezo wa 2x optical zoom, dual pixel phase detection autofocus, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3400 mAh battery yenye teknolojia ya Fast charging (Quick Charge 4.0+).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS, sehemu ya USB Type-C 1.0 reversible connector, Infrared port.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Blue, White na Gold
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Toleo moja linayo Fingerprint Kwenye Kioo (Kwa Mbele), Kufungua simu kwa kutambua uso (Face ID), Toleo Lingine linalo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Xiaomi Mi 8

Bei ya Xiaomi Mi 8 ina anzia Yuan ya China CNY2,699 kwa simu ya Xiaomi Mi 8 yenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa 64 GB, ambayo ni sawa na Tsh 961,000 . Wakati simu ya Xiaomi Mi 8 yenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128 inauzwa kwa Yuan ya china CNY2,999, sawa na Tsh 1,070,000. Toleo la mwisho la simu ya Xiaomi Mi 8 yenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 256 inauzwa kwa Yuan ya China CNY3,299, sawa na Shilingi ya Tanzania Tsh 1,180,000.

Kwa upande wa simu ya Xiaomi Mi 8 Explorer Edition ambayo itakuwa na RAM ya GB 8 na ukubwa wa ndani wa GB 128, yenyewe itakuwa inauzwa kwa Yuan ya China CNY3,799 sawa na Tsh 1,353,000.

Kumbuka bei hizo zinaweza kubadilika kutokana na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha, pia bei inaweza kubadilika kutokana na viwango vya kodi ya nchi husika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use