in

Sasa Utaweza Kuangalia Fainali za UEFA Kupitia YouTube

Sasa fainali za kombe la UEFA Champions League ni kupitia YouTube

UEFA

Mpira wa miguu ni moja kati ya mchezo unaopendwa zaidi duniani na imekuwa ni kawaida kuangalia mchezo huu kupitia vingamuzi au channel mbalimbali za kulipia, lakini mwaka huu hali itakuwa tofauti kidogo. Fainali za UEFA Champions League zimekuwa zikirindima kila mwaka mwezi May na mwaka huu utaweza kuangalia mchezo huo unaotegemewa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mubashara kabisa kupitia mtandao wa YouTube.

Fainali hiyo kati ya timu za Liverpool na Real Madrid zitakuwa mubashara siku hiyo kupitia channel ya BT Sport’s YouTube channel. Zaidi ni kuwa fainali hizo zitaonyeshwa kwenye mfumo wa 4K, yaani maana yake ni kuwa kama una kifaa chenye uwezo wa 4K basi utaweza ku-enjoy mchezo huo utakao fanyika jumamosi ya wiki ijayo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

“Tumekuwa tunasema kuwa tunataka kufanya michezo ya hali ya juu kupatikana kwa watu wengi na kwa mara nyingine tena tutafanya fainali za UEFA Champions League na Fainali za Europa League kupatikana kuangalia mtandaoni bure,” Msemaji wa BT Sport alinukuliwa akisema.

Hata hivyo siku ya jana Channel hiyo ya Youtube ya BT Sports, ilionyesha mchezo wa fainali za Europa League mubashara kupitia channel yao hiyo. Kwa bahati mbaya video hiyo kwa sasa huwezi kuiangalia kama uko nchini Tanzania, lakini unaweza kutumia programu za VPN kuweza kuangalia video hiyo kwa nchi zilizo ruhusiwa. Baada ya kuinstall VPN kwenye Simu au Kompyuta yako unaweza kuangalia video kwa kubofya hiyo hapa.

Kama wewe ni mpenzi wa mpira wa miguu basi, endelea kutembelea Tanzania Tech, tutangalia uwezekano wa kuweka video hiyo hapa ili wote tuweze kufurahia mchezo huo wa fainali siku ya Tarehe 26 ya mwezi huu wa tano.

Sasa Utaweza Kuangalia Fainali za UEFA Kupitia YouTube
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

6 Comments