in

Tengeneza Tovuti Kupita Simu Yako kwa Kutumia App Hii

Tengeneza tovuti nzuri kwa kutumia simu yako ndani ya dakika moja

tengeneza tovuti kwa simu

Ukweli ni kuwa iwe ni mfanya biashara au hata mfanyakazi wa kampuni fulani tovuti ni kitu cha muhimu sana, tovuti ni kama utambulisho maalum wenye mkusanyiko wa taarifa zako za muhimu ambazo unataka kushiriki na jamii iliyo kuzunguka. Lakini kunatatizo, sio kila mtu anaweza kutengeneza tovuti, wengine hawana hata kompyuta za kuweza kuwasaidia kufanya hivyo. Lakini sasa suluhisho limepatikana.

Kampuni moja inayo chipukia ya nchini marekani inayoitwa Universe, imeanzisha njia mpya na rahisi ya kutengeneza tovuti kupitia simu yako ya mkononi. Njia hiyo ambayo inatumia programu au App maalum inakupa uwezo wa kutengeneza tovuti za aina mbalimbali kwaajili ya biashara, tovuti binafsi na tovuti nyingine kama hizo.

Kupitia App hiyo utaweza kutengeneza kurasa za tovuti yako pia utaweza kuweka link zako za mitandao ya kijamii pamoja na kuandika maelezo mafupi kuhusu wewe au biashara yako. Vilevile kupitia programu hii utaweza kutengeneza tovuti yenye domain au kioleo cha bure cha onuniverse.com yaani tovuti yako itakuwa na link kwa mfano tanzaniatech.onuniverse.com

Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

Mbali na hayo utaweza kuchagua domain ya kulipia na kuiweka sambamba na tovuti yako uliyo tengeneza kwa kutumia App hiyo, App hiyo ambayo kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa iOS inakupa vifaa mbalimbali vya wewe kuweza kutengeneza tovuti yako ndani ya dakika moja tu. Unaweza kuangalia tovuti niliyo tengeneza kwa simu kwa kubofya HAPA. Unaweza kupakua programu hiyo kwenye simu yako ya iPhone na kuanza kutengeneza tovuti yako kwa urahisi zaidi.

Kwa watumiaji wa simu za Android bado hakuna taarifa lini programu hiyo itakuja kwenye mfumo huo lakini tuendelee kusubiri pengine programu hii itakuja siku za karibuni na bila shaka tutakujuza kupitia hapa hapa Tanzania Tech.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments

  1. Habari! hongera kwa taarifa muhimu za kiteknolojia duani. Kuna tatizo kidogo kwenye app sijui kama naliona Mimi tu au hata watumiaji wengine..ninapofungua kurasa fulani haimalizi yote hadi mwisho yaani utapata maelezo ya mwanzo kisha utakuta sehemu maneno yamekatika. Au wakati mwingine unapoama kwenye kurasa nyingine inafeli na wakati mtandao upo stable. Asante kwa kazi njema!