WhatsApp Kuja na Njia Mpya ya Kusaidia Kubadilisha Namba

Sasa utaweza kuchagua kuwapa taarifa watumiaji pale unapo badilisha namba
WhatsApp kubadilisha namba WhatsApp kubadilisha namba

Mtandao maarufu wa WhatsApp kwa sasa unafanya majaribio ya sehemu mpya ambayo itakusaidia kuweza kubadilisha namba kwa urahisi tofauti na hapo awali. Sehemu hiyo itakuruhusu kuweza kubadilisha namba ikiwa pamoja na kukupa uwezo wa kutoa taarifa kwa watu kwamba umebadilisha namba.

Sehemu hiyo ambayo bado iko kwenye majaribio kwenye programu ya WhatsApp Beta, itakupa uwezo wa kuchagua kama unataka kutaarifu watu wote kwenye kitabu chako cha majina ndani ya programu ya WhatsApp au kama unataka kumpa taarifa mtu mmoja.

Hata hivyo sehemu hiyo mpya itakupa uwezo wa kurudisha meseji zako zote ambazo ulikuwa unachati hata kabla ya kubadilisha namba, huku meseji mpya zikitokea na kuonyesha kuwa mtumiaji amebadilisha namba.

Advertisement

Sehemu hii ni moja kati ya sehemu muhimu sana hasa kwa wale wanao tumia WhatsApp ya Biashara kwani itasaidia pale unapotaka kubadilisha namba utaweza kuwapa taarifa wateja wako na hii itasaidia sana kutokupoteza wateja wako pale unapo badilisha namba.

Kwa sasa sehemu hii bado iko kwenye majaribio, endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi pindi sehemu hii itakapo fika kupitia programu yako ya WhatsApp.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use