Apps# 6 Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Jaribu programu hizi mpya kwenye simu yako ya Android
Apps# 6 Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android Apps# 6 Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Habari na karibu tena kwenye makala hizi ambapo tunakuwa tukiangalia programu nzuri za Android ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako yenye mfumo wa Android, Vilevile tuna tumaini kuwa programu au App hizi zinaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine hivyo basi, bila kupoteza muda twende tuka angalie programu tulizo kuandalia siku ya leo.

1. Bienks Viewer

Bienks Viewer
Price: Free+

Hii ni programu mpya itakayo kusaidia kutumia instagram kwa namna ya kiipekee, programu hii itakuruhusu kuangalia kurasa za watu mbalimbali bila hata kupakua app ya instagram, mbali na hayo app hii itakuwezesha kufanya mambo mbalimbali kama vile kupakua au kudownload picha pamoja na Stores kutoka kwenye kurasa mbalimbali za instagram.

 2. Device Info : Hardware & Software

Hii ni programu nyingine mpya ambayo itakusaidia sana kuweza kujua sifa za undani za simu yako, kama ulikuwa unatafuta kujua sifa halisi za simu yako basi programu hii ni moja kati ya programu za muhimu sana kuwa nazo kwenye simu yako ya Android na uhakika utaifurahia.

Advertisement

3. Nell Music

Nell Music
Price: Free

Nell Music ni programu itakayo leta aina mpya ya kusikiliza muziki kupitia simu yako ya Android, Programu hii ni nzuri sana na italeta muonekano mpya wa sehemu ya muziki kwenye simu yako hivyo hakikisha una jaribu programu hii kisha tuambie kwenye maoni hapo chini.

4. Opera News – Trending news and videos

Opera News ni programu kutoka kampuni ya Opera yenye kisakuzi cha Opera na Opera Mini programu hii itakusaidia kuweza kupata habari mbalimbali kulingana na vitu anavyo pendelea kuangalia mtandaoni. Kizuri kuhusu programu hii ni kuwa itakupa habari zaidi kadri unavyo endelea kuitumia.

5. Hibernate – Real Battery Saver

Kama simu yako imekua na matatizo ya kuisha chaji kwa haraka basi jaribu app hii mpya ya Hibernate, App hii itakusaidia kutunza battery ya simu yako na uhakika ukitumia App hii utaona utofauti wa battery kwenye simu yako kwa kiasi kikubwa kwani app hii inasaidia kuzima programu zinazo tumia kiasi kikubwa cha chaji pale kioo cha simu yako kinapokuwa kimezimwa.

Na hizo ndio programu nilizo kuandalia kwa siku ya leo, kama una maoni ushauri au hata kama kuna app unahisi ni nzuri na ungependa tuwajuze wengine, unaweza kutuandikia hapo chini nasi tutaiweka kwenye makala ijayo ya App bora. Pia kama ulipitwa na app zilizopita unaweza kusoma hapa kujua app nyingine za kujaribu kwenye simu yako ya Android.

3 comments
  1. hongereni kwa kutujuza kwa yote mazuri naweza Pata application ya kuficha picha ambayo muonekano wake ni tafauti na hizi zingine

    1. Ndio ipo programu inayoweza kuficha picha na yenyewe ipo kama kikokotozi au calculator, ingia youtube, kisha tafuta “jinsi ya kuficha file za simu” utaona video ya kwanza ni ya Tanzania Tech utaweza kujifunza kwa urahisi.

  2. Habarini Tanzania Tech, je naweza pata application ambayo naweza unganisha simu ya mke wng na whatsapp sms zake na calling ziwe zinapitia kwangu kwanza afu ndo niziruhusu kwenda kwake au app yoyote yenye kufanya spy kwa mawasiliano ya mke wnf

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use