in

Cue Roboti Mpya Yenye Uwezo wa Kucheza Mpira wa Kikapu

Roboti hii inauwezo wa kutupa mipira kwenye kikapu bila kukosea hata kidogo

Roboti ya kucheza Mpira wa Kikapu

Siku za karibuni Roboti zinaonekana kushika kasi sana, huku mfumo wa AI au (Artificial Intelligence) ukitumiwa kuwezesha roboti hizo kufanya mambo ambayo pengine ni ya kushangaza angalau kwa sasa.

Wengi wetu tunaijui roboti inayoitwa sofia, hii ni roboti yenye uwezo wa kuongea na kufikiri kama binadamu roboti hiyo hutumia mfumo huo wa AI kufanya hivyo, hivi karibuni napo tumeona roboti ya Flippy yenye uwezo wa kupika burger nayo pia inatumia mfumo wa AI na sasa roboti nyingine hii ya CUE yenye uwezo wa kucheza mpira wa kikapu nayo pia inatumia mfumo wa AI.

Sasa tofauti na roboti nyingine zilizo tangulia kuzinduliwa, roboti hii ya CUE inatumia mfumo huo kuweza kutupa mipira kwenye kikapu bila kukosea hata kidogo. Roboti hiyo iliyotengenezwa na wataalamu kutoka kampuni ya Toyota inauwezo wa kutupa mipira hiyo kwenye kikapu na kupatia kwa asilimia 100 kwa mujibu wa video ya ushahidi hapo chini.

Roboti hii inaonekana kuwashinda wachezaji wazuri wa mpira huo wa kikapu kwa kutupa mipira yote 10 bila kukosea hata kidogo au bila mpira kugusa pembeni ya kikapu. Wataalam walio tengeneza roboti hiyo kutoka kampuni ya Toyota, wanasema wametumia teknolojia kadhaa pamoja na AI kufundisha roboti hiyo kutupa mipira hiyo kwa ufasaa kabisa bila kukosea.

Tigo Pesa Mastercard Kwa Manunuzi Mtandaoni

Kwa sasa roboti hiyo hai-tegemewi kucheza mchezo wa mpira wa kikapu na bado wafanyakazi hao wa kampuni ya toyota wamesema wanaendelea kuboresha roboti hiyo na labda siku za karibuni inaweza kucheza kabisa mpira wa kikapu na sio kutupa mipira hiyo pekee.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.