Sophia Roboti Kama Binadamu Iliyopewa Uraia wa Saudi Arabia

Roboti hii inauwezo wa kujifunza mambo mapya kadri siku zinavyokwenda
Sophia Roboti Sophia Roboti

Sophia ni roboti ambayo iko mithili ya binadamu ambayo imetengenezwa na kampuni maarufu ya utengenezaji wa roboti ya Hanson Robotics. Kampuni hiyo ina makao yake makuu huko Hong Kong na ni moja kati ya kampuni inazojulikana sana kwa utengenezaji wa roboti kama binadamu maarufu kama (humanoid robot).

Hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza rasmi kwa umma roboti kama binadamu iliyopewa jina la Sophia, kwa mujibu wa roboti hiyo Sophia aliwashwa rasmi tarehe 19 April mwaka 2015 na kwa kipindi chote hicho cha miaka miwili sophia alikuwa akifundishwa mambo mbalimbali.

Mbali na uwezo wake wa kuongea Sophia anauwezo wa kutambua mambo mbalimbali kama hali ya hewa pamoja na uwezo wa kuonyesha hisia kwenye uso wake yaani (facial expression). Kwa kutumia uso wake wenye sura ya muigizaji wa zamani Audrey Hepburn, Sophia anauwezo wa kuonyesha kama amekasirika, kama amefurahi na kama amenuna.

Advertisement

Kwa mujibu wa mtengenezaji wake David Hanson, Sophia ametengenezwa kwa kutumia teknolojia za (Artificial Intelligence) kwaajili ya kujifunza mambo mapya, (Visual Data Processing) kwaajili ya kuona pamoja na (Facial Recognition) kwaajili ya kutambua sura za vitu na watu mbalimbali.

Kwa sasa Sophia amepewa uraia wa nchini Saudi Arabia na ameingia kwenye rekodi ya kuwa roboti wa kwanza duniani kupewa uraia wa nchi. Sophia amekuwa akiojiwa kwenye mikutano mbalimbali na hivi karibuni roboti hUyo aliojiwa na Umoja wa Mataifa UN na kueleza kuwa yuko kutoa msaada kwa binadamu kutengeneza maisha ya badae.

Watu mbalimbali duniani wamekua na hisia tofauti kwa kusema kuwa roboti huyo hakutakiwa kutengenezwa akiwa na uwezo huo. Je nini maoni yako unaonaje kuhusu roboti hizi..? unahisi zinaweza kuja kuwa msaada kwa binadamu au adui kwa binadamu tuandikie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use