in

WhatsApp Kuja na Njia Mpya ya Kuzuia Kusambaza Meseji za Uzushi

Sehemu hiyo mpya itaonyesha ujumbe wa kuzuia kusambaza habari za uzushi

WhatsApp Kuja na Njia Mpya ya Kuzuia Kusambaza Meseji za Uzushi

WhatsApp imekuwa akifanyiwa maboresho mbalimbali ili kufanya programu hiyo kuwa bora zaidi, hivi karibuni njia mpya kabisa inakuja ambayo itasaidia kuzuia kusambaza meseji za uzushi kupitia programu za WhatsApp.

Kwa mujibu wa tovuti ya WABetaInfo, sehemu hiyo mpya inaweza kutoa ujumbe kama meseji unayotaka kumtumia mtu imeshatumwa mara nyingi, Yani hapa nazungumzia zile meseji ambazo hutumika na watu na kukwambia uzitume kwa watu wengine 10 au zaidi.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo ujumbe huu utatokea kwa aliye tuma meseji hiyo na kama utamtumia mtu nae pia ataona ujumbe huo, kwa sasa bado hakuna habari kamili kama sehemu hii itakuja lini kwenye programu za WhatsApp lakini habari kutoka tovuti hiyo zinasema kwa sasa WhatsApp inafanya majaribio ya sehemu hiyo.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Hizi Hapa Aina 3 za Telegram Bots Muhimu Kuzifahamu

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.