in

Game Mpya ya Harry Potter Kuja Kwenye Smarphone Hivi Karibuni

Furahia game mpya ya Harry Potter Hogwarts Mystery kwenye smartphone

Harry Potter Hogwarts Mystery

Habari njema kwa wapenzi wa game za kwenye smartphone, hivi karibuni utaweza kucheza game mpya ya Harry Potter kupitia simu yako ya mkononi yenye mfumo wa Android pamoja na iOS.

Game hiyo mpya ya Harry Potter: Hogwarts Mystery, ina tegemewa kutoka ikiwa ni video game ya kwanza ya Harry potter kutoka toka mwaka 2012, pia ni game ya kwanza ya Harry Potter kutoka chini ya kampuni ya burudani ya Warner Bros. Interactive Entertainment.

Kupitia Game hiyo mpya utapa nafasi ya kujifunza njia mbalimbali za kupambana na wachawi pamoja na kujifunza njia mpya za uchawi kupitia kwa walimu ndani ya chuo maalum cha uchawi.

Kwa sasa bado haijajulikana game hii inatoka lini lakini, kwa mujibu wa mitandao mbambali tegemea kucheza game hii kwenye simu yako siku za karibuni, endelea kutembelea Tanzania Tech tutaku fahamisha pale game hii itakapo toka.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Game Nzuri za Kucheza Kwenye Simu ya Android

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment