Kava la iPhone 7 lenye Uwezo wa Kuchaji Simu Yako

Hili ndio kava la iphone 7 kutoka kampuni ya Mophie’s lenye uwezo wa kuongeza chaji kwenye simu yako
Mophie iphone 7 Mophie iphone 7

Kampuni maarufu kwa utengenezaji wa vifaa vya simu janja (smartphone) Mophie, jana ilitangaza kuleta kava lake la kwanza lenye uwezo wa kuongeza chaji kwenye iphone 7, kava hilo lenye kuangeza chaji zaidi ya masaa 33 limetengenezwa kwa battery maalum ambayo inawezesha simu yako kudumu na chaji zaidi.

Ili kuchaji kava hilo pamoja na simu yako, kava hilo linakuja na chaji isiyo na waya (wireless) ambayo itakuwezesha kuchaji battery ya kisasa iliyoko kwenye kava hilo pamoja na battery ya kwenye simu yako ya iPhone 7.

Advertisement

Kava hilo la Mophie’s Juice Pack Air linauzwa sasa kwa kati ya dollar za marekani $99.95  na $100 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 220,000, unaweza kununua kava hilo moja kwa moja kupitia kwenye tovuti ya kampuni hiyo ya Mophie.com.

Kwa habari zaidi ya vifaa vipya vya teknolojia endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use