Njia Rahisi za Kuongeza Follower Kwenye Instagram

Kama umeanzisha akaunti mpya ya instagram fanya hatua hizi kuongeza Follower kwenye Akaunti yako
Kuongeza Follower Kuongeza Follower

Pale linapokuja swala zima la kutafuta masoko (social media marketing) au follower kwenye mitandao ya kijamii ukweli ni kwamba ni lazima uwe makini sana kwani usipo kuwa muangalifu utakuta unatumia hela nyingi ili kuongeza kiwango cha mauzo kwenye biashara yako, hivyo ni vyema kuanza na hatua fulani za kawaida au za bei nafuu (ninge pendekeza za bure) ili kuongeza kiasi cha mauzo kwenye biashara yako hiyo mpya au hata ya zamani baada ya hapo ndipo uwende kwenye hatua za kulipia (hapa ni baada ya kuongeza msingi wa biashara yako hiyo).

Ni kweli kwamba kwa sasa mahali pazuri pakuanzia katika swala zima la kutafuta masoko ni kwenye mitandao ya kijamii, Na pia vilevile tukija kwenye swala zima la mitandao ya kijamii wote tunajua kuwa Instagram ni moja kati ya mtandao bora sana wa kijamii kwa sasa hivyo Basi ili kufikia hatua fulani ya mwanzo ni vyema kufuata hatua hizi ili kuongeza follower kwenye akaunti yako mpya ya instagram au hata ambayo ilikwepo hapo hawali, hatua hizi ni za bure kabisa na nirahisi kuzifuata.

1.Tumia Hashtags (#hashtags)

Advertisement

Matumizi ya hash tags yameonekana kuongeza follower kwenye mtandao wa instagram mpaka asilimia 50% hivyo ni vyema kutumia hashtags pale unapokua unapost kwenye mtandao huo. Kumbuka kutumia hashtags zinazotumiaka kwa wingi na watu mbalimbali.

2.Like Picha za Watu Mbalimbali

Hii ni njia nyingine ambayo ukweli ni kwamba inasaidia sana, hakikisha una like picha za watu ndani ya nchi yako ili kupata wateja sahihi fanya kila siku angalau hata picha 50 za kwanza.

3.Tangaza Akaunti yako kwenye Mitandao mingine

Hii ni nzuri sana kwa mtu ambaye tayari alisha anza kutafuta masoko kwenye mitandao mingine kwani ni vyema kujulisha wateja wako kuwa sasa unayo akaunti kwenye mtandao wa instagram.

4.Komenti Kwenye Picha Mbalimbali za Watu

Hii ni njia ya kawaida ya kupata follower kwenye mtandao huu wa instagram. kumbuka kukoment kwenye picha za watu ambao unahitaji wawe wateja wako, unaweza kutafuta akaunti ya mtu anaefanya biashara kama yako kisha kwa makini elezea baadhi ya bidhaa anazopost mwezako bila kukashfu.

5.Post Kuanzia Saa 1pm (Mchana) Mpaka Saa 5pm (Jioni) Siku za Wiki

Saa saba ni mda mzuri wa kupost kwani mida hii watu wengi huwa ndio mida ya chakula cha mchana au hata wengine huwa ndio wamemaliza kupata chakula hivyo kupata muda wa kuangalia simu zao kabla ya kurudi kwenye majukumu ya siku. Kuanzia saa kumi na moja na kuendelea unaweza kuendela kupromot post yako kwa kushare kwenye mitandao mingine (facebook) magroup mbalimbali na akaunti za marafiki zako.

6.Kumbuka Ubora unazidi Wingi (quality beats quantity)

Hapa ninamaana kuwa ni bora kupost picha nzuri na zenye msaada kwa wateja wako kuliko kupost picha nyingi lakini ambazo hazina msaada wowote kwa wateja na watumiaji wa bidhaa zako. Pia unawea kupost hata post zenye kufurahisha ili kubadilisha mood za wateja wako wakati kwa wakati (Hakikisha unapost kitu chenye kufurahisha kweli au kama ni Pole, Shukurani au hata kingine chochote kumbuka tu kumaanisha unachokipost).

7.Hakikisha Bio (Biography) Yako Imekamilika

Ukitaka watu wakuone muaminifu nibora kujiweka kwenye mazingira ya uaminifu, hii pia inakuwa kwenye profile yako ya instagram kama unataka follower ambao kweli wanaweza kuwa wateja wa bidhaa yako hiyo ni vyema uwaweke wazi unachokifanya na njia rahisi ya kufanya hivi ni kwakutumia bio ya Profile yako kwani hii ndio njia ya inayoelezea kitu unachokifanya na pia namna ya kukupata kwa urahisi kwa kutumia Email, Namba za simu au hata pia kwa kutumia tovuti yako ambapo utaweza kuwapa wateja wako maelezo zaidi kuhusu bidhaa yako.

8.Uliza Maswali Kwenye Picha ya Post (Caption) Zako

Nivyema kuruhusu wateja wako kujadili kwa kujibu maswali mbalimbali ambayo unawauliza kwenye post zako mbalimbali, kumbuka tu kupost vitu vya msingi kama ilivyosema kwenye hatua namba (6) sita.

9.Pendelea Kupost kwa Wingi Siku za Jumapili

Jumapili ni siku ambazo mara nyingi watu wengi wanakua na nafasi kubwa ya kuingia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hivyo ni vyema sana kutumia wakati huu kwa kutafuta masoko kwenye mitandao nhiyo mbalimbali ikiwemo instagram.

10.Elewa Wateja Wako au Watu unao Taka Wakufollow

Kwenye swala la kutafuta masoko hakuna kitu muhimu kama kujua mtumiaji wa bidhaa yako ni nani, maana yake ni kwamba ni vyema kujua kuwa unataka watu wa aina gani wakufollow kwa kutafuta kwenye akaunti mbalimbali za watu wanaofanya biashara kama yakwako utaona baadhi ya watu ambao wanapenda bidhaa hizo hivyo wafollow nao wata kufollow back.

Hatua hizi bado ni nyingi sana tutakua tukiziongeza mara kwa mara hivyo endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

8 comments
  1. nlikuwa nauliza naweje kutengeneza YouTube channel na kuweza kulipwa nalipwaje na pia blog wanakulipaje ” Ahsante

  2. Comment*Nlikuwa nauliza nawezaje kutengeneza YouTube channel na malipo wanakulipa kwa njia gani na blog pia wanakulipaje No zangu 0676391915″ Ahsante

  3. naomba kuuliza ulipyaji wa mitandao unakuwadje alafdu nimetengeneza blog ila templat sijajua nazidownload wap nimesha jalibu sana ila maelezo na video nimezielewa no yangu ni 0625891840

    1. Soma makala ya jinsi yakutengeneza blog unaweza kutafuta jinsi ya kutengeneza blog hapo juu kwenye sehemu ya kutafuta.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use