Simu ya Google Project Ara Kutoka Hivi Karibuni

Simu ya Google Project Ara ni Simu ya Kisasa yenye Uwezo wa Kutumia Vifaa Tofauti.
googles_project_ara googles_project_ara

Kwa wale wasiojua project ara ni nini.. well project ara ni aina ya simu ambayo inatengenezwa na kampuni maarufu ya google, simu hii ambayo ni smartphone ina uwezo wa kutumia vifaa mbalimbali ambavyo unaweza kuvitoa na kuvirudisha vifaa hivi ni vile ambavyo kwenye simu za kawaida ni ngumu kuvitoa yani kama vile kioo cha simu yako, spika, kamera na vinginevyo.

Simu hii ilianza kutangazwa katikati ya mwaka jana ambapo ilisemekana kuwa simu hiyo ingetoka hivi karibu watengenezaji wa simu hiyo yani (Google) kupitia mkutano wake wa mwaka 2016 ujulikanao kama Google io ambao uliofanyika huko Amphitheater  mountainview huko California ili tangaza kuwa sasa simu hiyo iko tayari kutoka,  ikiwa imesha fanikiwa kutengeneza mfano wa simu hiyo Google ilitangaza kuwa simu hiyo itatoka rasmi mwanzoni mwa mwaka 2017 ambapo simu hiyo itakuwa tayari kuingia sokoni mwaka huohuo.

Advertisement

Kujua zaidi kuhusu Google Project Ara unaweza ukatembela website ya projectara.com au angalia video hiyo apo juu kujua zaidi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use