#Ni katika Wiki ya Ubunifu Tanzania (IWTz) 2026
Katika Wiki ya Ubunifu Tanzania (IWTz) 2026, Vodacom Tanzania imeonyesha mchango wa mtandao, ubunifu na ujasiriamali katika kufanikisha Dira ya Maendeleo Tanzania 2050. Tukio hilo limewakutanisha wabunifu, wajasiriamali, watunga sera, wawekezaji, vijana na wadau mbalimbali chini ya kauli mbiu: “Kutoka Matarajio hadi Mageuzi: Kuibua Njia ya Tanzania Kuelekea Ustawi Jumuishi.”
Vodacom imeshiriki katika mjadala kuhusu uchumi wa watengeneza maudhui, maonesho, mikutano na wadau na shughuli za kuelimisha kuhusu usalama wa mtandao.

Akizungumza katika mjadala wa watengeneza maudhui na majukwaa mtandaoni, Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma, alisema mtandao una thamani zaidi kupitia fursa unazowawezesha Watanzania kuzipata katika elimu, biashara na ubunifu.




Kupitia Vodacom Youth Base (VYB), kampuni inaendelea kuwawezesha watengeneza maudhui kubaki mtandaoni na kukuza shughuli zao za kidijitali. Ushiriki wa Vodacom katika IWTz 2026 unaunga mkono malengo ya Dira ya Maendeleo 2050 kupitia mageuzi ya kidijitali, uvumbuzi na ukuaji wa uchumi jumuishi.


