Tigo Tanzania Yabadilisha Jina Sasa ni "YAS" 1

Tigo Tanzania Yabadilisha Jina Sasa ni “YAS”

Kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania imebadilisha jina lake na sasa inajulikana kama YAS. Mabadiliko haya yanaashiria hatua mpya katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano nchini, ambapo kampuni hiyo inalenga kuboresha huduma zake na kuendana na mahitaji ya kisasa ya wateja.

YAS imetangaza mabadiliko ya jina kwenye bidhaa yake ya TIGO PESA ambayo kuanzia leo itakuwa ikiitwa MIXX BY YAS.

Mabadiliko haya yametangazwa na Uongozi wa Kampuni hiyo katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Dar es salaam leo mchana ambayo Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kampuni hii kubadilishwa jina katika miaka yake yote thelathini ya huduma Nchini Tanzania ambapo awali ilikua ikiitwa Mobitel (BUZZ), kisha TIGO na sasa ni YAS!

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows) 2
Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)
Next Post
Laptop za Mwaka 2021 Ambazo ni Bora Kwa Matumizi 2026 3

Laptop za Mwaka 2021 Ambazo ni Bora Kwa Matumizi 2026