Tatizo la WhatsApp : Ku-upload au Kudownload Picha na Video 1

Tatizo la WhatsApp : Ku-upload au Kudownload Picha na Video

Imebidi turudi hewani muda huu kuelezea tatizo ambalo linaendelea hadi sasa kwa programu za WhatsApp, kama umekua unashindwa ku-upload picha au kudownload picha kupitia app za WhatsApp na Instagram basi hili sio tatizo lako pekee.

Kupitia Akaunti ya Twitter ya Instagram, Facebook imewataarifu watumiaji wake kuwa inajua kuhusu tatizo hilo na inaendelea na taratibu za kurudisha programu hizo kama kawaida.

Kwa upande wa WhatsApp hadi saa 11 usiku kwa saa za Afrika mashariki, bado hakuna taarifa zozote lakini inaonekana hadi sasa tatizo hili bado linaendelea. Unaweza kuona pale unapo download picha utaletewa ujumbe wa ERROR na mara nyingine picha, video au Voice note zote haziwezekani kudownloadiwa.

Leo tarehe 4/7/2019 Saa 2:30 usiku, tatizo hili tayari limesha tatuliwa na watumiaji wote wa mitandao ya kijamii ya Instagram, Facebook pamoja na WhatsApp wanaweza ku-download pamoja na ku-upload picha.

Makala hii imeongezwa kuonyesha tatizo limesha rekebishwa na watumiaji wote sasa wanaweza kuendelea kutumia mitandao yote ya kijamii kama kawaida.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Hatimaye Sasa Pokea Taarifa za Simu ya Android Kwenye Windows 2
Hatimaye Sasa Pokea Taarifa za Simu ya Android Kwenye Windows
Next Post
Kampuni Yalipa Tsh Bilioni 4.2 Kwa Kumtag Kim Kardashian Instagram 3

Kampuni Yalipa Tsh Bilioni 4.2 Kwa Kumtag Kim Kardashian Instagram