Mfumo wa Windows 7 Kusitishwa Ndani ya Mwaka Mmoja

Watumiaji wana muda wa mwaka mmoja ku-update kwenda Windows 10
windows 7 kusitishwa 2020 windows 7 kusitishwa 2020

Ni wazi kuwa Windows 7 ni moja ya toleo la Windows ambalo hadi sasa linatumiwa na watu wengi zaidi. Kwa mujibu wa data mbalimbali, inasemekana takribani asilimia 42.8% ya vifaa vyote vinavyo tumia mfumo wa Windows vinatumia mfumo wa Windows 7.

Sasa pamoja na mfumo huu kuwa maarufu na kutumiwa na watu wengi zaidi, hivi karibuni kampuni ya Microsoft imetangaza kusitisha mfumo huo baada ya mwaka mmoja. Kwa mujibu wa ripoti hiyo hadi kufika tarehe 14 January mwaka 2020, watumiaji wote wa mfumo wa Windows 7 wanatakiwa kuwa wamesha sasisha (Update) mfumo mpya wa Windows 10 kwenye vifaa vyao.

Aidha ripoti hiyo inasema, mfumo huo wa Windows 7 hautakuwa na msasisho mpya ya ulinzi baada ya tarehe hiyo, hivyo kompyuta pamoja na vifaa vingine vinavyo tumia mfumo huo vitakuwa hatarini kiusalama na kuweza kutoa mwanya kwa wadukuzi kuweza kudukua vifaa hivyo kwa urahisi.

Advertisement

Microsoft imeongeza kuwa, itaendelea kutoa masasisho mapya ya ulinzi ndani ya miaka mitatu kwa wateja wake wa akaunti za kibiashara walio lipia, lakini ndani ya miaka hiyo mitatu bei ya kupata huduma hiyo itakuwa ikiendelea kupanda kwa kila mwaka mpaka miaka hiyo mitatu itakapo kamilika.

Mfumo wa Windows 7 ni moja kati ya mfumo ulioleta mafanikio makubwa kwa kampuni ya Microsoft, pia ni moja ya mfumo ambao unakubalika na kupendwa na watu wengi zaidi duniani kuliko mifumo ya Windows 8 na Windows 10 ambayo hadi sasa bado inalalamikiwa kwa kuwa na matatizo mbalimbali.

Lakini pamoja na hayo, “kila jambo zuri halikosi kuwa na mwisho” hivyo kama wewe ni mtumiaji wa mfumo wa Windows 7 basi unao muda wa mwaka mmoja kuweza kusasisha (Update) mfumo wa Windows 7 kwenda mfumo wa Windows 10.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use