Yote ya Muhimu Yanayotegemewa Kwenye Mkutano wa MWC 2019

Haya ndio mambo machache ya muhimu yanayotarajiwa kuanzia tarehe 20
mkutano wa MWC 2019 mkutano wa MWC 2019

Mkutano wa MWC 2019 unakaribia kuanza huko nchini Barcelona, mkutano hufanyika kila mwaka kwa lengo la kukutanisha watumiaji na watengenezaji wa bidhaa za kielektroniki za mawasiliano hasa simu kutoka kampuni mbalimbali.

Mwaka huu mkutano wa MWC 2019 unategemewa kuanza rasmi siku ya Jumatatu ya tarehe 25 ya mwezi huu February. Pamoja na kwamba mkutano huu unaanza rasmi wiki moja kutoka siku ya leo lakini baadhi ya makampuni yanategemea kuanza mkutano huo mapema zaidi kuanzia tarehe 20.

Sasa kutokana na hayo leo nimeona sina budi kukwambia yale yote ya muhimu yatakayo jiri kwenye mkutano huo ambao kwa namna moja ama nyingine kampuni nyingi zinategemewa kuzindua simu zake mpya za kuanza mwaka 2019. Basi bila kupoteza muda twende nikujuze zaidi.

Advertisement

Samsung

Kwa upande wa Samsung ni wazi hadi sasa unajua kuwa kampuni hiyo inategemea kuzindua simu zake mpya za Galaxy S10, Galaxy S10 Plus na Galaxy S10e. Simu hizi zinatarajiwa kuzinduliwa siku ya Jumatano ya tarehe 20 ya mwezi huu February, sambamba na simu mpya inayojikunja ya Samsung Galaxy F au Foldable.

Galaxy S10, Galaxy S10 Plus, Galaxy S10e

Kwa sasa bado hakuna uhakika kama Samsung itazindua simu hiyo inayojikunja kwaajili ya kuingia sokoni, au itaonyesha ni hatua gani imefikia katika kuleta aina hiyo mpya ya teknolojia ya simu zenye kioo kinachojikunja. Kujua yote haya tuungane kwenye uzunduzi huo mubashara kabisa kupitia hapa Tanzania Tech.

Xiaomi

Hivi karibuni kampuni ya Xiaomi imesemekana kuanza hatua ya kuja barani Afrika, lakini kwenye mkutano wa MWC 2019 Xiaomi inategemewa kuja na simu mpya ya Xiaomi Mi 9. Simu hii ni simu ya kwanza kutoka kampuni hiyo ambayo inasemekana kuja na kamera tatu kwa nyuma, pia kama ilivyo Samsung, Xiaomi nayo inategemea kuzindua simu hii siku ya tarehe 20 mwezi huu wa pili.

Mbali na hayo, baada ya kuanza rasmi kwa mkutano huo hapo tarehe 28, kampuni ya Xiaomi inatarajiwa kuzindua rasmi simu ya kwanza yenye mtandao wa 5G ya Xiaomi Mi Mix 3’s 5G.

Huawei

Kwa upande wa kampuni ya Huawei, kupitia mkutano wa MWC 2019 kampuni hiyo inatarajiwa kuonyesha simu yake mpya inayojikunja ambayo itakuwa na teknolojia mpya kama ile ya Samsung. Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, simu hiyo inatarajiwa kuwa na uwezo wa mtandao wa 5G, huku simu hiyo ikitarajiwa kuendeshwa na processor ya Kirin 980 chipset.

Huawei Folder Phone

Hata hivyo inasemekana kuwa simu hii itazinduliwa rasmi tarehe 25, siku ya kwanza ya mkutano huo utakao fanyika huko nchini Barcelona. Kujua zaidi kuhusu teknolojia za simu ambazo huawei watakazo onyesha hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech.

Nokia

Kwa upande wa Kampuni ya Nokia tarajia kuona simu mpya ya Nokia 9 au Nokia 9 Pureview kama inavyo julikana kwa jina lake kamili. Kama wewe ni msomaji na mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech najua utakuwa unajua mengi sana kuhusu simu, hii ikiwa pamoja na habari ya simu hii kuwa simu ya kwanza sokoni yenye idadi kubwa ya kamera kwa nyuma.

Kama kwa namna yoyote ulikuwa hujui, Nokia 9 inakuja na kamera tano kwa nyuma huku zote zikiwa zinafanya kazi kwa pamoja kukupa picha nzuri kwa wale wapenzi picha, mpaka sasa bado haijajulika uwezo wa kamera hizi hivyo hakikisha unajiunga nasi mubashara kwenye mkutano wa MWC 2019 ambapo wote kwa pamoja tutaweza kujua uwezo wa kamera hizo.

Picha Nokia 9 Pureview

Hata Nokia sio kampuni ya kwanza kuja na wazo la kutengeneza simu yenye kamera nyingi kwa nyuma, mwaka jana (2018) kampuni moja ilitangaza kuja na simu yenye kamera tisa kwa nyuma lakini kwa bahati mbaya hadi sasa bado simu hiyo haijaingia sokono ijapokuwa picha za simu hiyo bado zinaendelea kusambaa mtandaoni.

LG

LG imetangaza kuwa, simu mpya ya LG G8 ThinQ itazinduliwa rasmi kwenye mkutano wa MWC 2019, kwa mujibu wa GSMArena simu hiyo inasemekana kuja na teknolojia mpya ambayo inapatikana kwenye TV za LG, teknolojia ya OLED Speaker ambayo inatumika kutengeneza spika zilizopo chini ya kioo.

LG G8 Thin Q

Mbali na hayo inasemekana kuwa simu hii itakuja na uwezo wa mtandao wa 5G kama itakavyokuwa simu moja ya Samsung S10 pamoja na simu mpya ya Huawei.

Sony

Kampuni ya Sony inategemewa kuwepo kwenye mkutano wa MWC 2019, ambapo inategema kuzindua simu zake mpya za Xperia XA3, pamoja na Xperia XZ4.

Sony Xperia XA3

Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali mtandaoni, Sony Xperia XZ4 na 10Z zinatarajiwa kuwa na vioo vyembamba na vikubwa, kamera tatu kwa nyuma pamoja na sehemu ya fingerprint ambayo inasemekana kuwa kwa pembeni.

https://tanzaniatech.one/finder/specs/sony-xperia-xa3/

Kampuni Nyingine

Oppo

Kampuni nyingine zinazo tarajiwa kuwepo kwenye mkutano wa MWC 2019, ni pamoja na kampuni ya Oppo ambayo inategemea kuonyesha teknolojia mpya ya kamera yenye uwezo wa ku-zoom mara nyingi zaidi kuliko kamera zote za simu duniani.

OnePlus

OnePlus inategemea kuonyesha aina mpya ya teknolojia yake ya 5G ambayo inategemewa kutumiaka kwenye simu zake zitakazo kuja kwenye miaka ya karibuni. Kwa sasa bado hakuna ripoti kama kampuni ya OnePlus itazindua simu mpya yoyote.

Vivo

Kampuni ya Vivo inatarajia kuwepo kwenye mkutano huo, huku ikitarajiwa kuonyesha simu yake mpya ya vivo V15 Pro simu ya kwanza kutoka kampuni hiyo yenye kamera inayo funguka kwa juu au (Pop up Camera).

Honor

Kampuni ya Honor nayo inasemekana kuwepo kwenye mkutano huo na inasemekana inatarajiwa kuzindua simu mpya ya Honor Magic, Simu ambayo inasemekana kutumia mtandao wa 5G. Hata hivyo kwa mujibu wa GSMArena simu hiyo inasemekana kuwa maalum kwa nchini china pakee.

Na hayo ndio machache ambayo pengine utegemee kuyaona kupitia mkutano wa MWC 2019 kuanzia hapo tarehe 20. Kwa habari zaidi kuhusu mkutano huu hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kujua yote ya muhimu yatakayo jiri kwenye mkutano huo, pia unaweza kupitia ukurasa wetu wa MWC 2018 ili kujua yote yaliojiri kwa mwaka jana kwenye mkutano huo.

1 comments
  1. naomba msaada wenu nnatumia simu ya Samsung Duos S3 nataka muito wa Meseji kuwa nyimbo ama niongeze ringtone za meseji nilizodownload naon amn iyo system

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use