Hatimaye Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A8s

Hii hapa ndio simu ya kwanza kuwa na kamera juu ya kioo
Sifa na Bei ya Galaxy A8s Sifa na Bei ya Galaxy A8s

Baada ya kusikia tetesi kuhusu ujio wa simu mpya ya Samsung Galaxy A8s, hatimaye simu hiyo leo imezinduliwa rasmi huko nchini China. Galaxy A8s inaingia kwenye rekodi kwa kuwa simu ya kwanza kuwa na kioo cha kisasa cha Infinity-O display pamoja na kamera ya kisasa ambayo ipo juu ya kioo.

Kampuni ya Samsung imeishinda kampuni ya Huawei ambayo nayo inajiandaa kuja na simu yake ya Honor View 20 ambayo nayo inategemewa kuja na kioo cha teknolojia hiyo pamoja na kamera iliyoko juu ya kioo.

Advertisement

Tukiangalia sifa za Galaxy A8s, Simu hii inakuja na kioo cha Inch 6.4 chenye resolution ya 1080 x 2340 pixels pamoja na uwiano wa 19.5:9. Simu hii inakuja na kingo nyembamba sana kiasi cha kufanya simu hii ionekane kama imetengenezwa kwa kioo kitupu.

Hatimaye Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A8s

Galaxy A8s inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya  Snapdragon 710 chipset ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 6 au GB 8. Simu hii pia inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 128 ukubwa ambao unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi ya GB 512.

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu, kamera moja ikiwa na Megapixel 24 ambayo hii ndio kamera kuu na kamera nyingine zikiwa na Megapixel 10 na Megapixel 5, Kwa mbele Galaxy A8s inakuja na kamera ya Selfie yenye uwezo mkubwa wa hadi Megapixel 24.

Hatimaye Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A8s

Galaxy A8s inaendeshwa na mfumo wa Android 9.0 (Pie) mfumo ambao juu yake kuna mfumo wa samsung experience 10. Battery ya simu hii inauwezo wa 3,400 mAh ambayo pia inakuja na teknolojia ya kuchaji kwa haraka hadi asilimia 50 kwa dakika 30. Sifa nyingine za Galaxy A8s ni kama zifuatazo.

Hatimaye Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A8s

Sifa za Samsung Galaxy A8s

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM710 Snapdragon 710 (10 nm).
 • Uwezo wa GPU – Adreno 616.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 512.
 • Ukubwa wa RAM –  RAM ya GB 6 au GB 8
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye f/2.0, 20mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 24 yenye f/1.7 na nyingine inakuja na Megapixel 10 yenye AF na kamera nyingine ina Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3400 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE, EDR pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO. USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Blue, Gray na Green.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy A8s

Kwa upande wa bei bado hakuna taarifa kamili kuhusu simu hiyo itauzwa kwenye nchi gani na itakuwa bei gani. Kupata taarifa zaidi endelea kutembelea makala hii tutaweka bei pale itakapo tangazwa rasmi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use