Jinsi ya Kuforward Simu Moja kwenda Nyingine (Kudivert)

Code za muhimu za kusaidia kufanya Call forwarding
Jinsi ya Kuforward Simu Moja kwenda Nyingine (Kudivert) Jinsi ya Kuforward Simu Moja kwenda Nyingine (Kudivert)

Kuna wakati unakuta labda uko mbali na simu yako au kwa namna moja ama nyingine unataka pale mtu aunapo kupigia simu kwenye namba yako moja aweze kukupata kwenye namba nyingine. Kama ulikua unataka kufanya hayo kwenye simu yako basi makala hii itaenda kukuonyesha njia hizo bila kutumia programu yoyote.

Mbali na hayo kama ulikuwa unataka ku-forward SMS kutoka kwenye simu moja hadi simu nyingine pia unaweza kusoma makala yetu ya apps nzuri ambazo zinaweza kukusaidia kufanya hivyo kwa urahisi zaidi, unaweza kusoma makala hiyo hapa. Basi baada ya kusema hayo twende sasa tukangalie code hizi.

Kumbuka baadhi ya mitandao ya simu hapa Tanzania huitaji laini inayo pokea simu inayo forwardiwa kuwa na angalau kuangia Tsh 100 na kuendelea, pia kama unataka kupokea simu ambayo imeforwardiwa unatakiwa simu ambayo imeforward iwe na salio kuanzia Tsh 100 na kuendelea. Kifupi ni kuwa unatakiwa kuwa na salio kwenye simu zako zote ili njia hii kufanya kazi.

Advertisement

Code za Ku-Forward Simu za Sauti

  • *21* Namba ya Simu # – Code hizi zinasaidia kuforward simu endapo simu yako itakuwa busy, haipatikani au haikupokelewa.
  • *67* Namba ya Simu # – Code hizi zinasaidia kuforward simu endapo simu iko busy tu, yaani hapa ni pale itakapokuwa inatumika au pale unapokata simu.
  • *61* Namba ya Simu # – Code hizi zinasaidia kufoward simu pale tu utakapokuwa hupokei simu yako, yaani simu pale simu inapoita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
  • *62* Namba ya Simu # – Code hizi zinasaidia kuforward simu endapo uko sehemu isiyo na mawasiliano au nje ya nchi mahali ambapo simu yako haishi mtandao.
  • *004* Namba ya Simu #  – Code hizi zinasaidia kuforward simu endapo uko busy, haupokei simu au kama uko sehemu ambayo haina mtandao vizuri.

Na hizo ndio code chache ambazo unaweza kuzitumia kwenye mtandao wowote kuweza kuforward simu. Kumbuka unatakiwa kuweka code hizi kwenye simu ambayo unataka kuiforward kisha sehemu ya namba weka namba ambayo unataka ipokee simu hizo.

Jinsi ya Kuondoa Call Forward Simu Zote (Mitandao Yote)

Kama kwa namna moja ama nyingine imetokea umaliza kutumia code hizo na unataka kuondoa code zote kutoka kwenye simu yako basi unaweza kubofya code hizo kwenye simu yako.

  • ##002# kisha kifute cha kupiga – Code hizi zitafuta simu zote zilizo forwardiwa na simu yako itarudi kupokea simu kama kawaida.

Kumbuka kama kwa namna yoyote umeshindwa kuondoa call forwarding, unaweza kuwasiliana na mtoa huduma kwa wateja wa mtandao unao utumia na atakuondolea call forwarding zote au atakupa maelezo jinsi ya kuondoa kwenye simu yako.

Hizi ndio code za muhimu za kuforward simu ambazo nimeona nishare na nyie, kama unataka maujanja kama haya unaweza kuendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku au hakikisha una tembelea kipengele cha Maujanja.

6 comments
  1. Maoni*AHSANTE KWA MAUJANJA ILA ME NATAKA KUDUKUA MAWASILIANO YA MPENZ WANGU YEYE AKIPOKEA NAME NISIKIE BILA KUTUMIA APP KAMAZIPO COD NISAIDIE MAJIBU HADHARANI
    UNAWEZA KUNITUMIA MAELEZO KUPITIA 0789338620

  2. Mimi nataka cod ambazo akipigiwa simu inaanza kufika kwangu kwanza ndo ifike kwake nijibu kwenye namba hiii 0763366675

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use