Twitter Kuja na Sehemu Mpya ya Kuzuia Watu Kujibu Tweet

Sasa utaweza kuchagua watu unaotaka waweze kujibu tweet zako
Twitter Kuja na Sehemu Mpya ya Kuzuia Watu Kujibu Tweet Twitter Kuja na Sehemu Mpya ya Kuzuia Watu Kujibu Tweet

Kama wewe ni mtumiaji wa Twitter kwa muda mrefu basi lazima unajua kuwa mtandao huo umekuwa ukitumika na watu mbalimbali huku sehemu ya reply ikiwa ni moja ya sehemu muhimu za pale mtu anapotaka kujibu tweet.

Lakini kuanzia siku ya leo Twitter inakuja na sehemu mpya ambayo itasaidia watumiaji kuweza kuzuia watu wengine kujibu tweet zao au kuchagua baadhi ya watu ambao wataweza kujibu tweet hizo.

Kwa mujibu wa blog ya Twitter, sehemu hiyo inategemewa kuanza kutumika kote duniani siku ya leo huku watu wote wakiwa na sehemu hiyo mpya ambayo itazuia watu wote au baadhi ya watu kujibu au ku-reply tweet mbalimbali.

Advertisement

Hivi ndivyo sehemu hiyo inavyofanya kazi. Kabla ya kutuma tweet, watumiaji watakuwa na chaguzi tatu za kuchagua nani anayeweza kujibu tweet.

Utaweza kuchagua sehemu ya kila mtu, ambayo ni sehemu ya kawaida, au utaweza kuchagua watu wanao kufuata ndio waweza kujibu tweet zako, au utaweza kuchagua watu unao wataka ndio wajibu tweet zako.

Unaweza kufanya hivyo kwa kuwatagi watu hao kwenye tweet hiyo au kuchagua watu pekee watakao weza kujibu tweet zako zote kupitia sehemu hiyo kwenye sehemu ya mpangilio au settings.

Twitter Kuja na Sehemu Mpya ya Kuzuia Watu Kujibu Tweet

Hata hivyo bado watumaji wataweza ku-retweet tweet yako, kutoa maoni au Comment, ikiwa pamoja na ku-link tweet yako na tweet nyingine. Pia twitter imeandika kuwa ukishiwasha sehemu hiyo kwenye tweet yako na kutuma tweet hiyo basi hutoweza kubadilisha.

Twitter Kuja na Sehemu Mpya ya Kuzuia Watu Kujibu Tweet

Kwa sasa sehemu hii tayari inapatikana kwa watumiaji wote hapa Tanzania na unaweza kupata sehemu hiyo moja kwa moja kwenye programu zote za Twitter za iOS na Android pamoja na tovuti ya Twitter.

Twitter Kuja na Sehemu Mpya ya Kuzuia Watu Kujibu Tweet

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kutufuata kwenye akaunti yetu ya Twitter ili kupata habari mpya pale zitakapo kuwa zinawekwa kwenye tovuti ya Tanzania Tech.

1 comments
  1. siku hizi mnaweza post chache chache sanaaaa, mimi napenda sana kujifunza vingi kutoka kwenu….ni mfuatiliaji mzuri mnoooooo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use