Game ya PUBG na App Nyingine 117 Zazuiwa Nchini India

Hadi sasa serikali ya India imefungia Apps 167 kutoka nchini China
Game ya PUBG na App Nyingine 117 Zazuiwa Nchini India Game ya PUBG na App Nyingine 117 Zazuiwa Nchini India

Wakati ikiwa bado China na Merakani zikiwa kwenye migogoro ya kibiashara, nchini India pia hali ya uhusiano wa China na India inaendelea kuharibika.

Baada ya serikali ya India kuzuia apps mbalimbali zaidi ya 58 za China kutumika nchini India, hatimaye hivi leo serikali ya India imetangaza kuzuia app nyingine 117 za China ikiwepo game maarufu ya PUBG.

Hadi sasa bado serikali ya india imesema sababu ya kuzuia apps hizo ni kutokuwa salama kwa matumizi ya wananchi wake. Hadi sasa India inakuwa imezifungia jumla ya apps 167 kutoka nchini China.

Kwenye list hiyo, app nyingine maarufu ukitoa game ya PUBG ni pamoja na Rise of Kingdoms, Art of Conquest, Arena of Valor na nyingine. Kwa mujibu wa tovuti ya Beebom, hadi sasa bado game hizi na baadhi ya app zinafanyakazi kwenye simu za watu waliokuwa wamepakua app hizo nchini India, lakini pengine hiyo inaweza isiendelee kuwa hivyo kwa muda mrefu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use