Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Itakayo Fanikiwa Mtandaoni

Hatua za muhimu ili kutengeneza tovuti itakayo fanikiwa mtandaoni
Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Itakayo Fanikiwa Mtandaoni Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Itakayo Fanikiwa Mtandaoni

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kuanzisha tovuti mpya basi hii ni makala ambayo na uhakika itakusaidia sana, pia kama unataka kujifunza tu natumaini makala hii itaweza kukupa elimu ambayo itakusaidia baadae pale utakapo fikiria kuanzisha tovuti yako ya kwanza.

Kabla ya kuendelea, ni vyema ufahamu kuwa kila mtu anayo nafasi mtandaoni na unatakiwa tu kuwa na ubunifu ili kuweza kufanikiwa mtandao. Huitaji mtaji mkubwa kuweza kuanza bali hakikisha unapofanya kitu mtandao unakifanya kwa ustadi na umakini wa hali ya juu huku mawazo yako yakiwa kwenye kusaidia jamii ya watu walio kuzunguka. Baada ya kusema hayo basi twende moja kwa moja kwenye makala hii ya leo.

Advertisement

Fahamu Maswali Yanayoulizwa Zaidi Mtandaoni

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Itakayo Fanikiwa Mtandaoni

Japokuwa internet imajaa mambo mengi ambayo sio mazuri, lakini pia ipo nafasi kubwa ya mambo mazuri hasa kwa jamii ya kitanzania. Hapa na maanisha kuwa, asilimia kubwa ya mambo ambayo watu hutafuta mtandaoni sio mambo mazuri lakini pamoja na hayo yapo mambo ambayo ni mazuri ambayo yanaweza kukusaidia sana kutengeneza tovuti itakayo fanikiwa.

Ili kutengeneza tovuti hiyo, hatua ya muhimu ni kujua matatizo ya jamii iliyo kuzunguka, matatizo ambayo yana hitaji ufumbuzi kupitia mtandao. Kama jamii iliyo kuzunguka inataka sana kujua zaidi kuhusu nyumba za kupanga basi ni nafasi yako kutengeneza tovuti ya nyumba za kupanga na kwa njia hiyo unaweza kufanikiwa kiarahisi.

Usifikirie Sana Pesa, Saidia Jamii Yako Kwanza

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Itakayo Fanikiwa Mtandaoni

Asilimia kubwa ya tovuti za kitanzania ambazo mimi binafsi nimekutana nazo mtandaoni zote huangalia zaidi Pesa, japokuwa pesa ni kiungo muhimu sana na pengine ndio lengo.. lakini sio mara zote kuwa na kiu ya pesa kunaweza kukusaidia kufanikiwa kimaisha. Hii ni muhimu kwa sababu ukiangalia sana pesa kuna wakati utashindwa kabisa kuendelea kutokana na kukosa pesa kwa muda mrefu hasa pale unapokuwa una anza.

Ni muhimu kuweka lengo la kusaidia jamii yako, au kusogeza huduma karibu na watu kuliko kufikiria zaidi pesa ambapo hii itafanya ufanisi wako kupungua pale pesa inapo pungua au kukosekana. Tovuti bora ni ile inayotoa mafunzo kwa jamii bia kujali pesa au malipo yanayo kuja kutokana na kazi hiyo, “siku zote ukifanya kitu kizuri pesa itakuja tuu… niamini mimi“.

Weka Nia Unapotaka Tovuti yako Kufika, Kuwa na Lengo

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Itakayo Fanikiwa Mtandaoni

Ukweli ni kwamba, siku zote biashara yoyote isiyokuwa na malengo huishia kufilisika au kufungwa. Hii ni kweli hata kwenye upande huu wa kutengeneza tovuti. Ni muhimu kufikiria au kuwa na maono ya wapi unapotaka kuwepo kwani hiyo itakusaidia sana sana sana.. Kwa maneno mengine ni muhimu kuwa na mfano wa tovuti ambayo imefanikiwa kwani hii itakupa nguvu na hari ya kutaka kufanikiwa zaidi kila siku.

Kwa mawazo yangu, ukweli ni kwamba pasingekuwa na ushindani katika dunia hii na uhakika kusingekuwa na watu wenye mali zaidi kuliko wengine. Na hakika watu waliofanikiwa walikua na angalau watu ambao walikuwa wana wafuatilia zaidi na kupendelea kuwa kama wao. “Ni vizuri kuwa na hari kwani kawaida hari ya kendesha tovuti inatokana na nia ambayo wakati mwingine huletwa na ushindani”.

Tengeneza Tovuti Bora na Rahisi Kutumia

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Itakayo Fanikiwa Mtandaoni

Mwisho ni muhimu kutengeneza tovuti ambayo ni bora na ambayo ni rahisi kutumia kwa watu wote. Kifupi ni kwamba wengi wa watumiaji wa hapa Tanzania wanapenda tovuti ambazo ni rahisi kutumia na ambazo zina muonekano mzuri. Ukweli ni kwamba Google pamoja na kampuni nyingine kama Bing huwa zina angalia pia muonekano wa tovuti yako, kwani mara nyingi muonekano pia unaweza kupandisha sana brand yako.

Brand yako huanza kwa muonekano na baadae kufuata jina pamoja na aina za makala ambazo unatengeneza. Ni muhimu kujenga muonekano bora kwa watumiaji kwani hii itasaidia watu kuamini zaidi tovuti yako ikiwa pamoja na kampuni yako. Pia usisahau kutengeneza tovuti ambayo ni rahisi kutumia kwani watumiaji wengi kupendelea zaidi tovuti ambazo ni rahisi kutumia.

Hitimisho

Kwa kufuata hatua hizo zote za awali na uhakika utakuwa uko njiani kuelekea kwenye mafanikio ya kufanikiwa kwenye mtandaoni. Kama unataka kujua njia za awali za kufanikiwa kwenye biashara mtandaoni basi unaweza kusoma makala yetu iliyopita hapa. Pia hakikisha una subscriber kwenye channel yetu ya Tanzania Tech kuweza kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments
  1. App iko vizuri, ila nahitaji kujua tofauti iliyopo kati ya app, blog, na website.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use