Tetesi : Kampuni ya Tecno Kuja na Simu Mpya ya Tecno Spark 2

Jiande na toleo jipya la simu mpya ya Tecno Spark 2 mwezi ujao
Tecno Spark 2 Tecno Spark 2

Simu janja ya Tecno Spark ni moja kati ya simu ambazo ziliuza nakala nyingi sana kwa mwaka 2017, Simu hiyo ilionekana kupenda zaidi sio kwa hapa Tanzania bali hata kwa nchi za jirani kama Kenya pamoja na Nigeria. Hata hivyo kama ilivyo kawaida ya kampuni ya Tecno, simu hii pia ilikuwa ni bora sana kwa upande wa kamera na imeonekana kushindana na simu nyingi za bei nafuu na kuendelea kubaki kwenye nafasi yake hadi sasa.

Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali kutoka mtandaoni, Kampuni ya Tecno inajiandaa kuzindua toleo jipya la simu hiyo toleo ambalo litakuwa na mamboresho mbalimbali pamoja na uwezo mzuri zaidi wa kamera kama ilivyo tamaduni ya kampuni ya Tecno. Wakati hizi zikiwa ni tetesi za awali, Tecno Spark 2 inatarajiwa kuja na kioo cha inch 6 chenye aspect ratio ya 18:9 display, vilevile tetesi hizo zinasema kuwa simu hii itakuja na teknolojia mpya ya kufungua simu kwa kutumia uso yaani face unlock.

Mbali na hayo, inasemekana kuwa Tecno Spark 2 itakuja na matoleo mawili, moja ya matoleo hayo kutakuwa na Tecno Spark 2 yenye kutumia mfumo wa Android Go, mfumo unaojulikana kutumika kuendesha simu za bei nafuu na zenye uwezo mdogo wa RAM ya kuanzia hadi GB 1 hivyo ni wazi toleo hilo litakuwa na RAM ya GB 1. Hata hivyo inasemekana kuwa toleo lingine la Tecno Spark 2 litakuwa na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16.

Advertisement

Kwa upande wa kamera inasemekana Tecno Spark 2 itakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 8, huku kwa nyuma ikiwa na kamera ya Megapixel 13 huku kwa pembeni kukiwa na sehemu ya ulinzi ya Fingerprint. Tetesi hizo zinasema kuwa Tecno Spark 2 inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao na inakadiriwa bei ya simu hiyo itakuwa kuanzia shillingi za Tanzania, Tsh 400,000 mpaka 350,000.

Kwa habari zaidi kuhusu simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tutakupa taarifa zaidi pindi tu tutakapozipata.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use