Tetesi : Sifa Zinazo Tarajiwa Kwenye Tecno Camon X (2018)

Sasa inasemekana simu hiyo itakuja na kamera mbili kwa nyuma
Tecno Camon X Tecno Camon X

Kampuni ya Tecno iko mbioni kuzindua simu yake mpya ya Tecno camon X, simu hii inatarajiwa kuzinduliwa hapo kesho kutwa tarehe 5 ya mwezi huu ambayo itakuwa ni siku ya Alhamisi. Hata hivyo uzinduzi rasmi wa simu hii umepanga kufanyika huko nchini Nigeria ambapo inasemekana simu hiyo itazinduliwa ikiwa imeboreshwa zaidi kwenye upande wa kamera.

Pamoja na kwamba tayari tumesha sikia tetesi kuwa simu hii inasemekana kuja na kamera kubwa ya kuanzia Megapixel 60, lakini wataalamu wa mambo wanadai kuwa tetesi hizo sio za kweli na badala yake simu hiyo inasemekana kuja na kamera mbili kwa nyuma ambazo zitakuwa na uwezo wa Megapixel 12 pamoja na Megapixel 20. Tetesi hizo pia zinadai kwa mbele simu hiyo ya Tecno Camon X itakuja na kamera mbili ambazo zitakuwa na uwezo wa Megapixel 8 kila moja huku zikiwa na falsh ya LED flash.

Haijaishia hapo, Tetesi hizo pia zinadai kuwa simu hiyo itakuja na ukubwa wa ndani wa aina mbili, yaani itakuwepo simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 16 pamoja na nyingine ambayo itakuwa na ukubwa wa ndani wa GB 32. Pia kwa upande wa mfumo simu hiyo inasemekana itakuja na mfumo mpya wa Android Oreo 8.1 mfumo ambao utakuwa ukisaidiwa na RAM kati ya GB 3 au GB 4.

Advertisement

Kioo cha simu hii pia kimetajwa kwenye tetesi hizo, ambapo inasemekana kioo cha Tecno Camon X kitakuwa na ukubwa wa Inch 5.99 huku kikiwa na teknolojia za Full-HD pamoja na IPS Display. Mengine yanayo tarajiwa kwenye Tecno Camon X ni pamoja na Fingerprint scanner, Mfumo mpya wa kupooza simu, Bluetooth 4.2, Laini mbili za simu au Dual SIM, uwezo wa 4G LTE pamoja na battery yenye uwezo wa 4000mAh ambayo itakuja na teknolojia ya quick charge.

Kwa upande wa aina ya Processor na aina ya Graphics au GPU bado haijajulikana hivyo itakubidi kusubiri mpaka kesho kutwa ili kuweza kujua sifa kamili za simu hiyo mpya. Kwa sasa bado hizi ni tetesi hivyo sifa kamili za simu hii zinaweza kuwa zaidi ya hapo au kuwa tofauti baada ya simu hii kuzinduliwa rasmi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use