Popular Now
Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026 1

Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra 2

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini 3

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini

Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 4

Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019

App namba moja kwa huduma ya muziki barani Afrika, Boomplay imemtaja msanii Diamond Platnumz, kuwa ndio mwanamuziki aliyesikilizwa zaidi Tanzania, kulingana na taarifa rasmi za muziki mwaka 2019.

Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye ripoti maalumu kuhusu muziki imeegemea zaidi data kutoka kwenye app hiyo ya muziki ambayo ina watumia zaidi ya milioni 60, ulimwenguni kote huku Tanzania kukiwa na watumiaji zaidi ya milioni 4.2. Boomplay inajivunia kuwa na aina tofauti za nyimbo ambazo idadi yake ni zaidi ya milioni 20, ambazo zinapatikana kwenye iOS, Android na web.

Nafasi ya pili imenyakuliwa na mwanadada Nandy, na ya tatu kuangukia kwake Harmonize huku Rayvanny akishika namba nne. Nae Aslay amekamata namba tano, huku namba sita ikinyakuliwa na Mbosso. Jux nae akainyakua nafasi ya saba huku Lava Lava akiijaza namba nane, mwanamuziki pekee wa injili katika orodha hii ni Joel Lwaga aliyeshika namba tisa na namba kumi akisimama mwanadada shupavu Vanessa Mdee.

Mbali na wasanii, Boomplay pia imekusanya taarifa kuhusu nyimbo ambazo zimesikilizwa zaidi pamoja na albamu, ambapo wimbo wa Diamond Platnumz akiwa na Fally Ipupa ‘Inama’ ndio umetisha zaidi kwa mwaka 2019. Albamu ya Nandy ya “The African Princess” imeshika nambari moja, huku “The Love Album” ya Jux ikishika namba mbili na kufuatiwa na “A Boy From Tandale” ya Diamond Platnumz iliyoangukia namba tatu.

Boomplay pia imetoa taarifa za mwenendo na tabia za namna muziki unavyosikilizwa Tanzania. Katika taarifa hiyo maalumu, Nyimbo Za Injili (Gospel) zimeonekana kusikilizwa zaidi na kufuatiwa na miondoko ya Bongo Flava, kisha Afrobeats inashika namba tatu, huku ya nne na tano zikishikwa na Hip Hop & Rap pamoja na Reggae.

Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 5 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 6 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 7 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 8 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 9 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 10 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 11 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 12 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 13 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 14 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 15 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 16 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 17 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 18 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 19 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 20 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 21 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 22 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 23 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 24 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 25 Takwimu za Muziki Kutoka Boomplay kwa Mwaka 2019 26

Previous Post
Movie Nzuri za Kuangalia na Familia Christmas Hii 27

Movie Nzuri za Kuangalia na Familia Christmas Hii

Next Post
Samsung Kuja na Galaxy Note 10 Lite na Galaxy S10 Lite 28

Samsung Kuja na Galaxy Note 10 Lite na Galaxy S10 Lite