Tetesi : TECNO na Infinix Kuingia Kwenye Biashara ya TV

Bado haijathibitishwa TV hizo zitazinduliwa lini, Ingawa inasemekana ni mwaka huu
Tetesi : TECNO na Infinix Kuingia Kwenye Biashara ya TV Tetesi : TECNO na Infinix Kuingia Kwenye Biashara ya TV

Baada ya kampuni ya Nokia kutangaza kuingia kwenye biashara ya TV hivi karibuni, hatimaye sasa kampuni nyingine za Infinix na TECNO nazo zimetarajiwa kutangaza kuingia kwenye biashara ya TV baadae mwaka huu 2020.

Kwa mujibu wa tovuti ya 91mobiles ya nchini India, brand hizo mbili ambazo zinamilikiwa na kampuni ya Transsion Holdings ya nchini China, zina tegemea kuleta TV za kisasa (smart TV) ambazo zitakuwa zikitumia mfumo wa Android.

Kwa mujibu wa tetesi hizo, Brand ya Infinix inategemewa kuja na TV zenye mfumo wa Android za kuanzia inch 43, huku kampuni ya TECNO yenyewe pia ikitarajiwa kuja na TECNO smart TV.

Advertisement

Tetesi : TECNO na Infinix Kuingia Kwenye Biashara ya TV

Hata hivyo, inasemekana kuwa kampuni ya Infinix ndio itakuwa ya kwanza kutoa TV zake na inasemekana kuwa TV hizo zita anza kupatikana kwanza kwenye soko la India kupitia masoko mbalimbali ya mtandaoni.

Kwa mujibu wa tovuti ya 91mobiles, inasemekana kuwa tayari kampuni ya Infinix ilishaanza kufanya maandalizi ya uzinduzi wa TV hizo mwezi january mwaka huu 2020, lakini kutokana na kusambaa kwa virusi vya corona duniani, kampuni hiyo ilisitisha tangazo hilo.

Hadi sasa bado hakuna taarifa za lini kampuni hizo mbili zita tangaza ujio wa TV hizo, au TV hizo zitakuwa zinapatikana kwa nchi gani nyingine ukiacha India.

Mbali na hayo, Pia hakuna taarifa za zaidi za sifa za TV hizo ingawa taarifa zainasema kuwa Smart TV ya Infinix inatarajiwa kupatikana kwa bei nafuu kuanzia Rupee ya India Rs 20,000 hadi Rs 25,000. Sawa na takribani Shilingi za Tanzania TZS 609,000 hadi 762,000 bila kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use