Simu 5 Unazoweza Kununua Sasa kwa Bei ya Chini ya TSh 350,000

Simu hizi unaweza kununua hapa Tanzania kwa bei nafuu sana
Simu 5 Unazoweza Kununua Sasa kwa Bei ya Chini ya TSh 350,000 Simu 5 Unazoweza Kununua Sasa kwa Bei ya Chini ya TSh 350,000

Wakati tukiwa tayari tunaendelea kwenye nusu ya pili ya mwaka 2019, zipo simu nyingi sana ambazo tayari zipo sokoni ambazo zinapatikana kwa bei nafuu kwa mwaka huu, sasa wewe kama mmoja wa watu ambao wanataka kununua simu mwezi huu najua ungependa kujua simu hizo ili kujipanga mapema kumiliki mmoja ya simu hizo.

Kupita makala hii nitaenda kukujulisha simu mbalimbali ambazo unaweza kuzipata sasa kwa bei nafuu ya chini ya shilingi za kitanzania TSh 350,000. Simu hizi tumezichagua kutokana na ubora wake pamoja na unafuu wake wa bei, pia unaweza kuzipata simu hizi sehemu yoyote Tanzania kwa kufuata maelezo mafupi. Najua una haraka ya kupata simu bora kwaajili yako na bila kuendelea kupoteza muda let’s get to it..

TECNO Spark 3 Pro

Simu 5 Unazoweza Kununua Sasa kwa Bei ya Chini ya TSh 350,000

Advertisement

Spark 3 Pro ni moja ya simu bora sana kwa sasa, simu hii ina ubora wa hali ya juu kiasi kwamba hii ndio itakuwa simu ya kwanza kutoka kampuni ya TECNO kupata mfumo mpya wa Android 10 Q ambao kwa sasa bado uko kwenye hatua ya majaribio. Mbali na kutambuliwa na Google, kampuni ya TECNO kupitia TECNO Spark 3 imeshinda tuzo ya Africa Information Technology & Telecoms Awards (AITTA) tuzo ambazo zimetolewa siku za karibuni huko nchini Nigeria.

Sifa za TECNO Spark 3 Pro

 • CPU: Quad-core 2.0 GHz
 • RAM: 2 GB
 • Storage: 32 GB
 • Kioo: IPS LCD, 6.2 inches
 • Kamera: Mbili Nyuma 13 MP, 2 MP
 • OS: Android 9.0 (Pie)
 • Bei: Tsh 280,000

Samsung Galaxy A10

Simu 5 Unazoweza Kununua Sasa kwa Bei ya Chini ya TSh 350,000

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Samsung na ungependa kuwa na simu bora ya Samsung kwa bei nafuu basi Galaxy A10 ni simu nzuri sana kwako. Simu hii ni moja kati ya simu za bei nafuu sana kutoka Samsung lakini pia ukifanikiwa kushika simu hii unaweza kusema ni simu ya Laki 8 au hata zaidi. Simu hii ina muundao wa kisasa na ukweli inapendeza sana ikiwa mkononi.

Sifa za Galaxy A10

 • CPU: Octa-core 1.6 GHz
 • RAM: 2 GB
 • Storage: 32 GB
 • Display: IPS LCD, 6.2 inches
 • Camera: 13 MP
 • OS: Android 9.0 (Pie)
 • Bei: TSh 280,000

Infinix Smart 3 Plus

Simu 5 Unazoweza Kununua Sasa kwa Bei ya Chini ya TSh 350,000

Infinix Smart 3 Plus ni simu bora ya bei nafuu kutoka Infinix, japo kuwa sio simu pekee ya bei rahisi kutoka kampuni hiyo, lakini Smart 3 Plus ni simu bora ya kuwa nayo kama unataka simu bora kwa bei nafuu. Simu hii inakuja na kioo kikubwa na pia inakuja na kamera tatu kwa nyuma ambazo zinaweza kukupa picha bora kama wewe ni mpenzi wa picha.

Sifa za Infinix Smart 3 Plus

 • CPU: Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53
 • RAM: 2/3 GB
 • Storage: 16/32 GB
 • Display: IPS LCD, 6.2 inches
 • Camera: Triple 13MP, 2MP, QVGA
 • OS: Android 9.0 (Pie)
 • Bei: Tsh 270,000

Infinix Hot 7

Simu 5 Unazoweza Kununua Sasa kwa Bei ya Chini ya TSh 350,000

Infinix Hot 7 ni simu nyingine bora na ya bei nafuu kutoka kampuni ya Infinix, Simu hii ni bora sana kwa uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu pamoja na kupiga picha nzuri za Selfie. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unataka simu ya bei nafuu yenye kudumu na chaji kwa muda mrefu, pamoja na kupiga picha za selfie vizuri basi hii ndio simu ya kununua kwa sasa.

Sifa za Infinix Hot 7

 • CPU: Quad-core 1.3 GHz Cortex-A7 (32nm)
 • RAM: 1/2 GB
 • Storage: 32 GB
 • Display: IPS LCD 6.2 Inch
 • Camera: 13 MP
 • OS: Android 8.1 (Oreo)
 • Bei: TSh 225,000

Infinix Hot 6x

Simu 5 Unazoweza Kununua Sasa kwa Bei ya Chini ya TSh 350,000

Infinix Hot 6x ni simu nyingine kutoka kampuni ya Infinix ambayo nayo pia ni simu bora inayo uzwa kwa bei nafuu, simu hii kama ilivyo simu iliyo tangulia nayo inasifika zaidi kwa uwezo wake wa kudumu na chaji kwa muda mrefu. Hot 6x inakuja na battery kubwa ya 4000mAh ambayo inaweza kudumu na chaji kwa siku moja nzima kutegemeana na matumizi yako.

Sifa za Infinix Hot 6x

 • CPU: Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53 (28nm)
 • RAM: 3/2 GB
 • Storage: 32 GB
 • Display: IPS LCD 6.2 Inch
 • Camera: Dual 13 MP, 2 MP
 • OS: Android 8.1 (Oreo)
 • Bei: TSh 320,000

Na hizo ndio simu bora za bei nufuu ambazo unaweza kuzipata kwa sasa, kama unataka kujua sehemu za kununua simu hizi unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutakusaidia kupata simu hizi kwa bei hizo zilizo andikwa.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tutakujuza yote kuhusu simu, kompyuta, programu, na mengine mengi. Kama unataka kujifunza maujanja mbalimbali hakikisha una subscribe kwenye channel yetu hapa na uhakika hotojutia.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use