TECNO Inakukuaribisha Tena Kwenye Ulimwengu Mpya wa Phantom

Mbali ya kuja na simu mpya ya Phantom, pia TECNO inakuja na kauli mbiu mpya
TECNO Inakukuaribisha Tena Kwenye Ulimwengu Mpya wa Phantom TECNO Inakukuaribisha Tena Kwenye Ulimwengu Mpya wa Phantom

Kauli ya mgeni njoo, mwenyeji apone imedhihirika baada ya ujio wa simu za Phantom kutoka TECNO mobile. Ni moja kati ya simu pendwa miongoni wa watumiaji wa simu za TECNO toka mwaka 2015. Nini hasa kinafanya matoleo ya Phantom kuteka soko zaidi.?

Mara zote Phantom hua inatolewa kila mwaka ikiwa imeshiba specifications na features kali kuliko!. Ilikua ikisemekana kwamba kwakua mwaka jana TECNO hawakutoa toleo la Phantom, kampuni hiyo ilikua inafanya utafiti na kujipanga kuleta simu ambayo itakua ipo vizuri kwenye kila sekta.

TECNO Inakukuaribisha Tena Kwenye Ulimwengu Mpya wa Phantom

Advertisement

Tetesi hizo ziligundulika kua ni za kweli baada ya kampuni kuzindua simu hiyo mpya ya Phantom 9 mwezi huu huko nchini India. Uzinduzi huo ulienda sambamba na kampuni kutangaza kuongeza mkataba wa ushirikiano wao na klabu kubwa Uingereza ya Manchester City, pamoja na kubadili kauli mbiu yao kutoka “Experience more” kwenda “Expect More”, yaani ikimaanisha ‘tarajia zaidi’.

TECNO Inakukuaribisha Tena Kwenye Ulimwengu Mpya wa Phantom

TECNO Inakukuaribisha Tena Kwenye Ulimwengu Mpya wa Phantom

Dhima kuu ya kauli hii ni kuwahakikishia watumiaji wa simu za TECNO juu ya ubora na uimara zaidi utakaoletwa na kumpuni hii pendwa nchini na kwenye bara kwa ujumla. Kwa sasa, TECNO inashika nafasi ya 5 Afrika kama kampuni ya simu inayopendwa zaidi.

Nisikuchoshe sana, hakika simu hii imekuja na muundo wa kipekee na mzuri zaidi wa kuvutia. Kamera tatu za nyuma, kamera ya mbele, kioo kikubwa na kizuri zaidi chenye muundo wa “dot notch” kwa juu pale katikati.

Tumekua tukiona makampuni mengi ya simu yakiondoa tundu la kuchomeka earphone; lakini hapa kwenye Phantom 9 TECNO wameona watuachie “earphone jack” ambayo ipo upande wa chini wa simu hiyo.

We unaona ni jambo gani limekuvutia sana kutoka toleo hili? Endelea kutufuatilia kwa ajili ya kupata sifa nyingine nyingi pamoja na maelezo ya undani kabisa kuhusiana na TECNO Phantom 9.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use