Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu za Bei Nafuu Kuanzia TSh 300,000 Kushuka Chini

Kama unatafuta smartphone ya bei nafuu ya kununua soma listi hii
Simu za Bei nafuu Simu za Bei nafuu

Kuwa na smartphone kwa sasa ni kitu cha muhimu sana, iwe wewe ni mfanyakazi au mwanafunzi au hata mfanyabiashara simu ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku.

Kuliona hilo leo Tanzania Tech tumekuletea list ya simu za bei nafuu, simu hizi unaweza kuzinunua sasa hivi kupitia maduka mbalimbali na kwa tathmini tulio ifanya simu hazito zidi Tsh 300,000 za Tanzania. Kama umekuwa ukitafuta simu za bei nafuu kwa muda mrefu list hii itaweza kusaidia sana kupata simu nzuri na ya bei nafuu ili uweze kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki. Basi kabla sijakuchosha tuangalie list ya simu hizi za bei rahisi.

Advertisement

1. Samsung Galaxy Grand Prime Pro

Hii ni simu ya Samsung ambayo pengine ni ya bei nafuu zaidi, simu hii inakuja na sifa za kawaida na ni simu nzuri sana kwa matumizi yote ya kawaida.

Sifa za Galaxy Grand Prime Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.0 cha Super AMOLED
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.1 (Nougat)
  • Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 GB
  • RAM –  GB 1.5  au GB 2 (kwa India)
  • Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 2600mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 300,000

2. TECNO Spark 2

Tecno Spark 2 ni moja kati ya simu ambayo tumeiongelea sana hapa Tanzania Tech, simu hii ina muonekano mzuri sana na ukweli simu hii inadhamani sawa na pesa unayolipa.

Sifa za TECNO Spark 2

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 6.0 cha IPS LCD
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo (Go Edition)
  • Processor -Quad Core 1.3GHz
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 GB
  • RAM –  GB 1
  • Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 3500mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 260,000

3. NOKIA 2

Nokia 2 ni simu nyingine ambayo ni bei nafuu, simu hii inakuja na muonekano mzuri sana pamoja na sifa nzuri kwa bei rahisi. Simu hii inapatikana sasa kwa bei rahisi sana.

Sifa za Nokia 2

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.0 cha LTPS IPS LCD
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.1.1 (Nougat) inatarajiwa kupata Android 8.1 Oreo
  • Processor – Quad-core 1.3 GHz Cortex-A7
  • Ukubwa wa Ndani – GB 8
  • RAM –  GB 1
  • Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 4100mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 239,000

4. Infinix Hot 6

Simu hii ya infinix Hot 6 pia sio simu ambayo ni mara ya kwanza tunaiongelea hapa Tanzania Tech, Simu hii pia ni simu ya bei nafuu na unaweza kuipata sasa kupitia maduka mbalimbali.

Sifa za Infinix Hot 6

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 6.0 cha HD+ IPS LCD
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo
  • Processor – Quad-core 1.4GHz
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16
  • RAM –  GB 2
  • Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio (Bado Haija Thibitishwa), Inayo Fingerprint
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 280,000

5. Samsung Galaxy Prime Plus

Galaxy Grand Prime Plus ni simu nyingine ya bei nafuu kutoka kampuni ya Samsung, simu hii inakuja na muonekano na sifa nzuri kwa gharama nafuu.

Sifa za Galaxy Grand Prime Plus

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.0 cha PLS TFT
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0 (Marshmallow)
  • Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53
  • Ukubwa wa Ndani – GB 8
  • RAM –  GB 1.5
  • Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 2600mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 283,000

6. TECNO Pouvoir 1

Kama kweli unatafuta simu ya bei nafuu na yenye ubora basi Tecno Pouvoir 1 ni simu nyingine ambayo unaweza kuipata kwa gharama nafuu sana.

Sifa za Tecno Pouvoir 1

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.5 cha IOS LCD
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
  • Processor – Quad-core MediaTek Mt6580
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16
  • RAM –  GB 1
  • Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 5000mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 270,000

7. Nokia 3

Nokia 3 ni simu nyingine ya gharama nafuu sana na simu ambayo ni nzuri kwa muonekano pamoja na sifa. Simu hii imezinduliwa hivi karibuni na imeshafika hapa Tanzania na unaweza kununua kupitia maduka mbalimbali.

Sifa za Nokia 3

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.0 cha IPS LCD
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.1.1 (Nougat) inatarajiwa kupata Android 8.1 Oreo
  • Processor – Quad-core 1.4 GHz Cortex-A53
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16
  • RAM –  GB 2
  • Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 2630 mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 299,000

8. TECNO F2

Simu nyingine mpya ya bei nafuu kwenye list hii ni Tecno F2, Simu hii inakuja na muonekano mzuri sana pamoja na sifa nzuri sana.

Sifa za Tecno F2

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.0 cha FWVGA IPS
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
  • Processor – Quad-core 1.3GHz
  • Ukubwa wa Ndani – GB 8
  • RAM –  GB 1
  • Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 2000mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 200,000

NUNUA HAPA KWA TSH 169,000

9. TECNO Spark K8

TECNO Spark K8 ni simu nyingine nzuri na ya bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno, Simu hii inapatikana kwa bei rahisi sana na inakuja na sifa nzuri.

Sifa za Tecno Spark K8

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.5 cha HD IPS
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
  • Processor – Quad-core 1.2 GHz
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16
  • RAM –  GB 1
  • Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 3000mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 290,000

10. TECNO Camon CX Air

Sidhani kama nina haja ya kusema mengi kuhusu simu hii, ukweli ni kuwa simu hii ni simu ya bei nafuu sana na inapatikana kwenye maduka mengi sana hapa Tanzania. Sifa za simu hii ni nzuri sana na muundo wake pia ni mzuri sana.

Sifa za Tecno Camon CX Air

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.5 cha HD IPS
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
  • Processor – Quad-core 1.25 GHz
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16
  • RAM –  GB 2
  • Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 3200mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 295,000

11. TECNO WX4

Simu nyingine ya bei nafuu kutoka kampuni ya tecno ni WX4, Simu hii ni nzuri sana na ina uwezo mzuri na inakupa simu yenye thamani ya pesa yako. Simu hii inapatikana sasa kwenye maduka mbalimbali hapa nchini Tanzania na unaweza kuinunua leo.

Sifa za Tecno WX4

  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha Inch 5.0 cha HD IPS
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
  • Processor – Quad-core 1.3 GHz
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16
  • RAM –  GB 1
  • Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 2800mAh
  • Mengineyo – Inayo Radio
  • BEI – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 255,000

Na hizi ndio simu za bei nafuu ambazo unaweza kuzipata sasa kwenye maduka mbalimbali, Kama wewe ni mpenzi wa simu za Tecno unaweza kusoma makala hii hapa ya simu za bei rahisi za Tecno. Pia unaweza kusoma hapa kama unatafuta simu nzuri za Tecno zenye kamera nzuri. Kama hapo pia utakuwa hujapata simu nzuri ya kununua basi unaweza kusoma hapa kupata list ya simu za bei nafuu zinazouzwa chini ya Tsh 250,000.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use